Rais wa Singapore kuanza ziara ya kiserikali Tanzania kesho Juni 9, 2026

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Rais wa Jamhuri ya Singapore, Mheshimiwa Tharman Shanmugaratnam, anatarajiwa kuwasili Tanzania jioni ya leo kwa ajili ya kuanza Ziara ya Kiserikali kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kesho, Juni 9, 2026, Rais Shanmugaratnam atapokelewa rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam na mwenyeji wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi yatakayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Singapore katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji, maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi, pamoja na uchumi wa kidijitali.

Soma Pia: Rais Singapore anatarajia kufanya ziara nchini Tanzania tarehe 8/6/2026

Majadiliano hayo yatafuatiwa na utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

Screenshot 2026-06-08 182024.png
Screenshot 2026-06-08 182036.png
 
Amekuja kufanya nini hapa? Au naye anaua kama kawa! kwake huko.
Russia , China naweza nikamuelewa. Huko murder case inatumia less than 30 minutes na ananyongwa mtu!
 
Tunafanana nao kabisa...
Toka tupate uhuru ni chama kimoja tu kilichoshika dora cha CCM
Na Singapore toka wapate uhuru wanaongozwa na chama kimoja PAP.

Vyama vingine viko kama urembo tu kama hapa kwetu..
 
Rais wa Jamhuri ya Singapore, Mheshimiwa Tharman Shanmugaratnam, anatarajiwa kuwasili Tanzania jioni ya leo kwa ajili ya kuanza Ziara ya Kiserikali kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kesho, Juni 9, 2026, Rais Shanmugaratnam atapokelewa rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam na mwenyeji wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi yatakayolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Singapore katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji, maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi, pamoja na uchumi wa kidijitali.

Soma Pia: Rais Singapore anatarajia kufanya ziara nchini Tanzania tarehe 8/6/2026

Majadiliano hayo yatafuatiwa na utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

welcome to Tanzania president Tharman Shanmugaratnam:KasugaYeah:
 
Back
Top Bottom