Rais wa Somalia na Viongozi wa Upinzani Wasaini Makubaliano Mapya ya Uchaguzi

Rais wa Somalia na Viongozi wa Upinzani Wasaini Makubaliano Mapya ya Uchaguzi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamoud, pamoja na viongozi wakuu wanne wa upinzani, wamesaini makubaliano kuhusu uchaguzi ujao nchini humo. Makubaliano haya yaliyokamilika tarehe 25 Agosti 2025, yanabainisha mfumo mpya wa uchaguzi baada ya Bunge kupitisha sheria ya uchaguzi Oktoba 2024, ambayo inaleta utaratibu wa kura moja kwa kila mtu ifikapo mwaka 2026

Makubaliano hayo yanaweka kwamba Rais ataendelea kuchaguliwa na Bunge, huku wabunge wakichaguliwa kwa kura za moja kwa moja. Pia, vyama vya siasa vitakavyopata angalau asilimia 10 ya viti bungeni vitatambuliwa rasmi. Wadau wote wa kisiasa wamekubaliana kushirikiana kuelekea mfumo wa “mtu mmoja, kura moja,” hatua ambayo Rais Mohamoud ameielezea kama mwanzo wa ujenzi mpya wa taifa

Hata hivyo, makubaliano haya yameibua mpasuko ndani ya upinzani. Baadhi ya viongozi, akiwemo Rais wa zamani Sherif Sheikh Ahmed, wanaona hali ya usalama nchini bado haijawa thabiti kuendesha mageuzi makubwa ya uchaguzi. Hii inamaanisha kuwa licha ya mafanikio ya kisiasa kwa Rais Mohamoud, changamoto kutoka kwa upinzani uliogawanyika bado zitaendelea kuibuka

-----------------------------------

Somalia's President Hassan Sheikh Mohamoud and four key opposition leaders have signed an agreement concerning the upcoming elections in Somalia

The agreement, finalized on August 25, 2025, outlines the framework for the country's electoral process. This follows the adoption of a new electoral law by Parliament in October 2024, which establishes universal suffrage for the 2026 elections

While this reform is seen as a progressive step forward, it has faced considerable backlash from opposition members who are committed to the existing indirect clan-based system. President Mohamoud expressed optimism, stating, “The doors to state reconstruction are now open,” after two months of intense discussions that led to this agreement

Key elements of the agreement include the election of the President by Parliament, while Members of Parliament will be elected through a system of universal suffrage. Additionally, political parties that secure at least 10% of the parliamentary seats will gain official recognition. Crucially, all political actors have pledged to work towards the transition to a "one person, one vote" electoral system. However, this agreement has also exposed divisions within the opposition

Despite this victory for President Mohamoud, he may face ongoing challenges from a fragmented opposition, particularly from former President Sherif Sheikh Ahmed, who argues that Somalia's current security situation does not support such significant electoral reforms. Stay tuned for further updates on this developing story in Somalia

Source: Africa News, TRT Global, Somali Global
 
Waislamu huwa wananifrahisha sana unaweza kumuona mtu kila siku kavaa kanzu ukajua jamaa imani imepanda sana, KUMBE HANA NGUO ZA KUVAA
 
Somalia wamefanya reforms kabla hata ya tunaojiita kisiwa cha amani!! Sijui nani alituroga
 
Back
Top Bottom