Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemteua bila kukusudia mtu aliyekufa kuwa mjumbe wa kamati itakayoandaa uchaguzi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Msemaji wa ofisi ya rais amesema hii leo kwamba mamlaka zilipitiwa wakati wa uteuzi baada ya Steward Sorobia Budia, mwanasiasa wa zamani wa upinzani kuwa miongoni mwa wajumbe waliotajwa katika amri iliyotolewa na Kiir
Budia alifariki miaka mitano iliyopita.Taarifa zinasema familia ya marehemu sasa inadai fidia, kwa kuzingatia tamaduni zinazokataza kuomba au 'kuamsha' roho ya marehemu bila ufahamu, ridhaa au ushiriki wa familia.Sudan Kusini haijawahi kufanya uchaguzi tangu ilipopata uhuru 2011, na imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kila mara.