Shirika la Utangazaji la Sudan Kusini (SSBC) lilitangaza Jumatano kuwa Rais Kiir amemfutia kazi Semeya Kumba aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, pamoja na kumfuta kazi Atong Kuol Manyang aliyekuwa Waziri wa Biashara.
Hakuna sababu yoyote iliyotolewa kuhusiana na mabadiliko hayo, ambapo Kiir pia alimuondoa Mawien Mawien Ariik katika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Ndani (ISB) kwenye Kitengo cha Usalama wa Taifa, na kumteua Akec Tong Aleu kuchukua nafasi yake.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa Rais Kiir amekuwa akifanya mabadiliko ya mara kwa mara kwenye safu za jeshi na serikalini ili kuendelea kushikilia hatamu za uongozi, huku akikabiliana na migogoro ya silaha pamoja na tetesi zinazoendelea kuhusu nani atakayemrithi madarakani.
Soma pia Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amemfuta kazi Spika wa Bunge, Jemma Nunu Kumba pamoja na Naibu wake
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Source: Reuters