kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Ni vigumu kutambua nafasi ya Rais wa Tanzania hasa katima hoja aidha ni mwajiri wa wananchi au ni mwajiriwa wa wananchi.
Marais waliopita wametengeneza dhana kwamba wao ni waajiri wa wananchi huku wanapokuwa kwenye Mikutano ya adhara wakihubiri kwamba wao ni waajiriwa. Rais wa Tanzania anaogopwa na wananchi na awezi kukosolewa anapokwenda mrama, katika mazingira haya utabaini huyu siyo mwajiriwa Bali n mwajiri. Siku zote mwajiriwa umheshimu mwajiri lakini ukiona mwajiriwa anakosa nidhamu kwa mwajiri Basi amechoka kazi.
Kama tunakubaliana huyu Ni mwajiriwa Basi lazima tukubali kwamba anapaswa kukosolewa na kuondolewa madarakani pale inapoonekana afai kufanya kazi tuliyompa. Wananchi kushindwa kumkosoa Rais aidha kwa staha au bila staha Ni kielelezo Cha Rais kugeuka kuwa mwajiri wetu.
Niombe tuanze mchakato wa kujinasua mikononi mwa kuajiriwa na Rais, tuzinduke tuweke mkakati wakumwajiri Rais. Zuma, Trump na Marais wengine wa aina yao wameajiriwa na wananchi. Ni vigumu mtu mmoja kuajiri watu milioni 60+ , huyu ni mwajiriwa wetu na tunapaswa kumwajibisha anapokwenda kombo. Tudai katiba inayotupa mamlaka yakumwajiri Rais