Jeff Gemo
Member
- Jul 11, 2015
- 34
- 26
Salaam wana JF.
Tumekuwa na mijadala mingi juu ya uchaguzi wa TFF, tumetazama ahadi zao, mipango, sera na namna watakavyotekeleza. Kila mgombea ametoa ahadi zile zile anazoamini watu wangependa kuzisikia, na ndio uchaguzi ulivyo kote duniani. Binafsi sioni kama hivyo ni vigezo vya msingi sana kumpata Rais atakaeongoza TFF, tutaishia kulaumiana na kurudi tulipotoka. Kuwa na sifa za kugombea Urais sio sababu tosha ya kumfanya mtu kuwa Rais!
Hoja yangu kubwa ni kwamba, tuwapime kwa uwezo wao na kile walichokifanya badala ya maneno yao na kile wanatakachokifanya, nafasi ya Urais ni kubwa sana kuitoa kwa majaribio au mtu kujifunzia uongozi, wajumbe wa mkutano na wapiga kura ni vema mkalitambua hili ili mtupatie mtu sahihi anayeweza kuanza kazi siku ya pili baada ya kuthibitishwa kuwa Rais.
Wagombea wakubwa na wenye nguvu katika uchaguzi huu ni hawazidi wanne, na kati yao ni lazima tumpate Rais. Kwa mtazamo wangu nadhani ni vyema zaidi kama wajumbe wangejikita katika kutazama mazingira ya mpira wa sasa na uwezo wa wagombea kututoa hapa, wasitilie sana maanani maneno ya kampeni yanayozungumzwa kwasababu hata wasio na uwezo wa kuwa Marais wameongea maneno matamu na ya kuvutia.
Legend Ally Mayay “Tembele” ni mtu makini na ana sifa zote za kugombea Urais na ndio maana mamepitishwa katika nafasi hiyo. Mayay amekuwa mchezaji mzuri na sasa ni mchambuzi bora wa michezo, historia yake haioneshi kama amewahi kuwa kiongozi wa chama chochote cha Mpira Mkoa au wilaya, lakini wadau hawana shida na hilo, wanataka mabadiliko.
Mayay kama atachaguliwa kuwa Rais wa TFF hii ina maana kwamba atakuwa anajifunza uongozi na kupata uzoefu kupitia nafasi nyeti kabisa, nafasi ya juu nay a mwisho katika jedwali la uongozi wa TFF. Hatuwezi kufanya majaribio katika nafasi kubwa namna hii ndugu wajumbe, hatuwezi kutoa nafasi ya mtu kujifunza uongozi tena wenye changamoto kubwa na nzito kama TFF, tutarudi tulipotoka. Mayay ni kijana shupavu na anao uwezo na muda wa kujizoesha na kujifunza uongozi kupitia vyama vya mikoa na wilaya ili atakaposema “anataka kufanya makubwa” aeleweke kwasababu ameishi katika mifumo ya uongozi wa soka.
Fredrick Mwakalebela ni mgombea mwingine mwenye nguvu na uzoefu wa kutosha, amewahi kuwa kiongozi katika soka na serikali, sote hatuna shaka juu ya hilo. Ukakasi pekee ninaoupata ni mwenendo wake katika masuala ya uongozi na mashaka juu ya usimamizi wa fedha. Mwakalebela aliyekuwa katibu mkuu wa TFF mbali na kuhusishwa na rushwa katika harakati zake za kisiasa, bado alihusishwa na utapeli wa Shilingi milioni 30. Augost 23, 2011 Mwakalebela alisaini mkataba (pengine akijua anampiga Abdi Kassim) uliopelekea kufunguliwa kesi No OB/RB/16369/2014 katika kituo cha Polisi cha Oysterbay cha jijini Dar es Salaam.
Ikiwa huu ndio mtazamo wa Kiongozi wa TFF, ni nini tutakuwa tunafanya? Ni mabadiliko gani tutakuwa tunatafuta? Tunahitaji mtu anayeweza kudhibiti fedha na kusimamia wengine kikamilifu. July 2011, aliyekuwa Mkurugenzi wa Takukuru Dk Edward Hoseah alisema wazi kuwa walikamilisha kesi ya Mwakalebela, ambayo sijui iliishaje lakini inatosha yeye kuhusika na TAKUKURU kuthibitisha.
Kuwa na kiongozi mwenye makandokando ya namna hii ni kuhatarisha zaidi soka letu, mpaka Napata mashaka huenda hata uchaguzi huu tayari “kafanya mambo”. Mwakalebela amezoea kuwa kiongozi (unaweza kuwa ni uzoefu pia) nadhani baada ya kesi yake dhidi ya Mhe. Msigwa kutupiliwa mbali ameamua aingie TFF ili kubadili hali ya soka, lakini kesi zake na kuhusishwa kote na “Utapeli” bado hatujasahau na ninawaza akiwa Rais atafanya nini zaidi? Sidhani kama ni chaguo sahihi.
WALLACE KARIA, Huyu amekuwa sehemu ya Mfumo mbovu zaidi kuwahi kutokea katika soka la Tanzania, makamu wa Rais ambaye Rais wake ametufikisha hapa. Karia anaweza kuonekana ni “wale wale” kwasababu mfumo aliokuwa nao umekuwa na kashfa na kesi nyingi za ajabu ambazo zimepelekea Rais kushikiliwa na vyombo vya usalama.
Swali ninalojiuliza ni hili, kwanini Wallace Karia yupo Uraiani wakati Rais na Katibu mkuu wakishikiliwa? Swali linguine ni kwamba, Karia ameongoza kamati nyingi za fedha na amekuwa mweka hazina, lakini sijasikia kabisa akihusishwa na ubadhilifu, kwanini?
Baada ya Malinzi na katibu wake kutiwa mbaroni, alipigiwa simu Karia ili azungumzie hilo (kwasababu yeye ni makamu wa Rais haiwezekani asiwepo kwenye mpango huo wa pamoja) ajabu ni kwamba Karia alikuwa Morogoro na hakuwa akijua chochote juu ya ubadhilifu ule.
Ninachokiona ni kwamba Wallace Karia kacheza “disco” katikati ya matope na hajachafuka (nimeeleweka hapa), haiwezekani Karia awe safi wakati kiongozi wa juu na wa chini wamechafuka, huyu mtu ni muadilifu kwa kiwango gani???
Kwahiyo kuna maswali kama hayo unaweza kujiuliza na utaona ambavyo Karia amekuwa kiongozi imara na amesimama peke yake kwa nidhamu kubwa sana na uadilifu, amekuwa kiongozi mzuri kote alipopita na hakuna kashfa inayomfuata zaidi yah ii ya “Ukimbizi” ambayo nayo imeshatatuliwa.
Karia ni ameitumikia Serikali kwa umakini mkubwa, na pote alipohamishiwa kikazi basi alikwenda kubadili hali ya mchezo wa mpira wa miguu, mikoa mingine alisaidia mpaka kupandisha timu daraja, ameshindwa kuishi bila kujihusisha na michezo na zaidi sana ameshindwa kuvumilia soka linapokwenda.
Karia alichukua fomu ya Urais wakati ambao Jamal Malinzi nae amechukua, ni kwanini Karia aliamua kupambana na Jamal wakati walikuwa Ofisi moja?? Nadhani umepata picha ni kwa namna gani Karia amekuwa akikasirishwa na uongozi wa pale TFF, anaijua TFF vizuri, anawajua “wapigaji” kwa majina yao, na hatoruhusu wamzunguke akiwa Rais, hili linanipa imani kubwa kwamba anaweza kuwa Rais Mzuri na akatutoa hapa tulipo.
Kila mtu huwa na ile kiu ya kutaka kufahamu udani wa mgombea, na ikiwa kweli tunahitaji maendeleo ya mpira basi Wallace Karia ni chaguo sahihi, ana sifa nyingi za ziada kuliko wagombea wenzie wote, Ni mchapakazi na muadilifu wa vitendo na ndio maana hata wabaya wake wameshindwa kumpata na kashfa yeyote na hivyo ikabaki kusema sio Raia.
Nilisema hapo awali kwamba tuwapime wagombea wetu kwa kile walichokifanya kwanza kupitia uongozi badala ya kile watakachokifanya wakiwa viongozi, na nikasema pia nafasi ya Urais ni nyeti na wadhfa wa mwisho katika uongozi wa mpira wa miguu Tanzania, ni lazima Rais awe na historia ya kuongoza kwa mafanikio na kusimamia maslahi ya mpira wa miguu nchini.
Karia amekuwa Mkurugenzi wa wilaya tofauti katika utumishi wa serikali, lakini pia ameshika nafasi 12 za uongozi wa Mpira kwa nyakati tofauti, zikiwemo nafasi za utunzaji fedha na usimamizi, na nafasi kubwa zaidi ni Makamu wa Rais TFF. Kote huko Karia kapita salama bila kesi ya aina yeyote, ni nani mwingine zaidi yake??? Hakuna.
Hata kama wajumbe wataamua kutazama vipaumbele ambavyo mimi binafsi sioni kama ni tija sana, bado Karia ana vipaumbele vilivyosimama wima na amekuwa akikosa nafasi ya kuvitekeleza kwasababu hakuwa Rais, anayo masuala 11 aliyoyapanga kama kikosi kinachoanza katika mpira wa miguu, yote 11 yameshiba na yanatekelezeka ikiwa atapewa nafasi hiyo.
Wapiga kura tunawaomba sana mtuchagulie WALLACE KARIA awe Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), kwa sababu ndio mgombea pekee mwenye sifa zaidi ya tunavyohitaji, na amekuwa katika mfumo tunaouchukia ambao hata yeye anauchukia na anajua madhaifu yote na ndio maana alikuwa tayari kupambana na Jamal Malinzi katika kinyang’anyiro hiki, aliona wazi kuwa makamu wa Rais kusingeweza kumpa nafasi ya kubadilisha soka letu.
Ni imani yangu kwamba huko Dodoma ni jina la WALLACE KARIA ndio litashangiliwa baada ya kutangazwa kuwa Rais, nina imani na wajumbe wa mkutano huo ambao ndio wapiga kura kwamba hawatatuangusha, tunawatakia kila la kheri, hekima na busara ziwaongoze ili sisi sote kwa pamoja na WALLACE KARIA kama Rais wetu, tuinue hali ya soka nchini.
Time for Change.
Jeff Gemo Mnyama Machine
The One Man Army
Affirmative Gemo The Great!!
Maoni binafsi, uchaguzi TFF.