Rais wa TFF, Jamal Malinzi, kuzungumza na Vyombo vya habari Kesho Juni 23, 2015

Rais wa TFF, Jamal Malinzi, kuzungumza na Vyombo vya habari Kesho Juni 23, 2015

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi, kesho siku ya Jumanne tarehe 23 Juni, 2015 ataongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli ya Tansoma eneo la Gerezani - Kariakoo majira ya saa 5 kamili asubuhi.

Waandishi wote wa habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Baraka Kizuguto,
Media & Communication Officer
 
Kwa kweli tutamkumbuka Tenga, TFF ni Tenga na El-mmary tu waliweza kuimudu, hawa wengine wote ni wasanii.
 
Hawezi kujiuzulu...Atakuja na sound zingine za kipuuzi kama kawaida.

Na mitanzania tulivyo...Nothing will happen.

Mitanzania ndivyo tulivyo....Kwa hisani ya Nyani Ngabu.
 
ili washabiki wa soka la Tanzania tulidhike ni lazma malinzi ajiuzulu, la sivyo tutampindua kama nkurunzinza,, yaani malinzi ndio kaja kuua soka la bongo hao wengine wote wanasingiziwa
 
ili washabiki wa soka la Tanzania tulidhike ni lazma malinzi ajiuzulu, la sivyo tutampindua kama nkurunzinza,, yaani malinzi ndio kaja kuua soka la bongo hao wengine wote wanasingiziwa
Utaanzia wapi??! unaijua katiba ya FIFA? haikuwekwa vile ki bahati mbaya, ni makusudically, na ndio maana wanamtetea sana Blatter, ukihoji kidogo, ohho mambo ya mpira ni marufuku kupelekwa mahakamani!! ndicho kinachowapa kibuli. Tatizo la tz kila kitu tunataka kuleta usanii!! kuna vingine usanii haukubali!!! michezo ni maandalizi, bora hata nyambui, ameitwa huko BRUNEI, Kuwamkufunzi wa riadha na atakuwa chini ya wizara ya michezo ya huko, kwani hapa amechoka, michuano kesho, unapewa pesa leo kuandaa timu ya riadhaa, ikishindwa lawama ni kwako, pesa nyingi wamewekeza kwenye soka ambalo limetushinda, na ktk timu za east and central africa, taifa stars ndio timu pekee yenye ufadhiri mkubwa, lakini ndio timu bogus tena!!!!
 
Anataka kusema nni mpuzi huyu???
Yaani yupo pale lakini haelewi yupo pale kufanya nni.
 
Hivi katika ofisi za TFF hakuna ukumbi wa mikutano?
 
basi utasikia anawaomba radhi watanzania kwa kufungwa goli 13-0 mechi tano mfululizo.
 
Nakubaliana kabisa kuwa uongozi wa sasa wa TFF na sekta ya michezo kwa ujumla ni tatizo. Lakini ni sekta gani nchini ambayo haina matatizo? Taifa Stars ni kweli inafanya vibaya Lakini niambieni ni wapi tanzania tunafanya vizuri?
 
bila kubadilisha mfumo mzima na kuwa na mipango endelevu ya kisoka hasa kuanzia kwa vijana hata atawale nani yatabaki yaleyale.Tuamue kufuata principle halali za maendeleo ya football na tufute kabisa siasa michezoni.
 
Kama Na Yeye Anakuja Kusema Kuwa Anajiseppblater ( Kujiuzuru Urais Wake ) Tutamshukuru Ila Kama Anakuja Tu " KUZOZA " Kihaya Tutazidi Kumdharau Na Asipoangalia Atapopolewa Mawe.

Tumemchoka Jamal Malinzi Aungane Na Kocha Wake Mart Nooij Aliyefia South Africa Katika Mashindano Ya COSAFA Na Akaja Kuzikiwa Rasmi Zanzibar Katika Mashindano Ya CHAN.
 
" Watanzania tusidanganyane; Bila uwekezaji kwenye soka la vijana hatuwezi kufika popote " Jamal Malinzi, Rais wa TFF.Kikao ndio kimeanza
 
Back
Top Bottom