Rais wa TFF, Jamal Malinzi pamoja na Katibu Mkuu Celestine Mwesigwa washikiliwa na TAKUKURU

Tatizo ni uandishi au Tatizo ni nini mkuu? Sijakuelewa aisee, unaweza kunisahihisha pia
Umeandika kitu cha msingi sana. Sote kuna tunapotaka kuwa lakini kila mmoja anadhani njia yake ndio sahihi wakati tukishirikiana mawazo tutafika huko bila lawama au 'kuvutana mikia'!
 
A

Anaitwa Ally Mayai Tembele
Hivi yupo TRA au Wizara ya Viwanda na Biashara kama Afisa Masoko(?)
Ngoja watakuja kutusahihisha mkuu,tusubiri wenye uhakika
Mkuu barafu,Ally Mayai Tembele na mgombea aliyeko TRA ni watu wawili tofauti.
 
Mkuu barafu,Ally Mayai Tembele na mgombea aliyeko TRA ni watu wawili tofauti.
Nieleweshe mkuu wangu
Huyu Ally Mayai Tembele si ndiyo yule ukiwa nyumbani unatazama Azam Sports Xtra anafanyq uchambuzi wa habari za michezo?
Na si ndio huyu huitwa Ally Mayai?Aliyepata kuchezea Yanga na timu ya Taifa?Na husemwa kuwa ni mtumishi wa Wizara niliyotaja?
Je huyo wa TRA ni nani??nisaidie tafadhari
 
Yes, maelezo yako hayo yanamhusu Ally Tembele. Huyo wa TRA sina kumbukumbu ya jina lake, lakini niliona kwenye media baada ya kuchukua fomu walimtambulisha kama mfanyakazi wa TRA. Ana mwili sio kibaumbau kama Ally Tembele. Ukifuatilia hata google unaweza kupata jina lake
 

Tena kwa huyo ndo secretariat watapiga balaa yeye hajui, mwisho wa siku Rais unawajibika....
 
Nchi hii sometime unaweza kushindwa kuelewa wakati wa kuwa serious au wakati wa kutimiza 'melengo' fulani fulani. Sio ajabu ukasikia kuwa alijenga uwanja wa golf kijijini kwake kwa pesa za tff!
Mkuu huo uwanja umejengwa huko kijijini?
 
The safe place of Jamali Malinzi to life
protection is hell....
 



Baada ya habari kuenea katika mitandao ya kijamii kuhusiana na katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa na Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi wamekamatwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU, uthibitisho umetolewa kutoka ofisi ya TAKUKURU kitengo cha mahusiano.

Afisa mahusiano wa TAKUKURU Musa Misalaba ameongea na waandishi wa habari na kuthibitisha kukamatwa kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa lakini hawajataja sababu za kuwashikilia.

 

1.TBL baada ya kufanya ukaguzi ubadhirifu ulionekana wazi wazi ndio wakaamua mkataba ulivyoisha wakagoma kuongeza
2.Unajua gharama za kupanga ofisi PPF Tower kwa mwezi ukilinganisha na kukaa kwenye ofisi zao bure pale Karume ?
3.Stars kushuka viwango ni ufundi,Nani anaajiri makocha wa TFF ? Kwa nini alivyoingia alimfukuza kazi Poulsen na kumlipa karibia mil 200 na akaajiri makocha wabovu zaidi na baadae kamrudisha timu ya vijana

Nilishasema tangu mwanzo tuhuma unazifahamu lakini unajifanya huzifahamu,endelea kumpigia kampeni
 
hii habari inakanganya, mara wamekamatwa kwa mambo ya hongo mara ubadhirifu.
 
TAKUKURU wamechukua simu zao zote!!

Na hapo ndipo ' watakapoumbuka ' hasa kwa Jamal Malinzi ambaye hupenda mno kucheza michezo yake ya ' hatari ' kwa kutumia Simu. Mfano hai ni zile Simu zake alizokuwa akiwasiliana wakati wa ile mechi ya Geita FC ambapo ' mawasilino ' yake yalinaswa achilia mbali zile ' sms ' zake akitoa maelekezo ya ' matokeo ' pamoja na ' Maswahiba ' zake akina ' Matandika '. Huko katika hiyo Simu yake nina uhakika 100% PCCB watayakuta na mengineyo mengi tu.

Ally Mayai na Mzee wangu Mtemi Ramadhan haya sasa Majengo ya Karume yanawasubirini nyie tu mkatuongozee mpira wetu tafadhali.
 
Nasubiri reaction ya FIFA juu ya hiyo move ya takukuru kuingilia vyama vya hiari!! Sijui nani mshitaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…