Hzo zote ni dhana ndg. We umeona kuna ubaya gani kuhamisha ofisi za shirikisho? Matokeo yapi yaliyopangwa? Kushuka kwa viwango vya stars ni suala la ufundi, ndio maana wameona njia bora ya kunusuru soka letu ni kuwekeza kwa vijana kama walivyofanya wenzetu mataifa yaliyoendelea. Ubaguzi wa kikabila hata me sikubaliani naye, japo ipo hvyo taasisi nyingi tu duniani. Kuhusu ubadhirifu, siwezi kusema chochote maana me sijaona ushahidi wowote wa kudhihirisha hayo. Jambo lingine muhimu ni kujua kuwa maamuzi ya raisi wa shirikisho ktk mambo ya ufundi sio wa mwisho. Kuna kamati ya utendaji na sekretarieti yake ambazo zinafanya kazi nyingi sana kwa pamoja.