Rais wa TFF Wallace Karia atembelea Kambi ya Yanga SC kushuhudia mazoezi ya klabu hiyo

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Wallace Karia ametembelea Kambi ya Yanga Avic Town na kushuhudia mazoezi ya klabu hiyo kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zalan FC utakaofanyika kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam

Karia kwenye mazungumzo yake na kikosi hicho, amesema kuwa ana hakika kuwa timu hiyo itafanya vizuri kwa namna alivyowaona wakicheza mechi za Ligi, huku akiviombea vilabu vya Tanzania kushinda michezo yao na akitaka nafasi nne Kimataifa zilindwe.

"Nataka hizi nafasi nne Kimataifa tuzilinde" amesema Wallace Karia

 
Mwanaume kapambana sasa hivi Tanzania inapeleka team nne halafu misekule ya hersi inauliza simba ana mafanikio gani kimataifa wakati hizo nafasi nne hamna point moja ya utopolo hapo.
 
Mwanaume kapambana sasa hivi Tanzania inapeleka team nne halafu misekule ya hersi inauliza simba ana mafanikio gani kimataifa wakati hizo nafasi nne hamna point moja ya utopolo hapo.
Ndo maana akasisitiza nafasi nne Kimataifa zilindwe..!
 
Karuhusiwa na nan huyu msomali?viongozi wa yanga sometime wanafanyaga u.k.m kweli
 
Bora tu wangemfungia geti, ili ijulikane moja. Ana nongwa sana huyu jamaa dhidi ya Yanga.
Angeenda zake Malawi kwa wale ndugu zake, hakuna ambaye angeshangaa.
Thubutu yao, kuna mwenye uwezo wa kumfungia geti hapo.! huyu ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania.

Kipindi kile tunawaambie kuwa kuna vitu haviendi sawa kwa Karia, hasa ule mkataba wa GSM mlisema lolote?

Tulieni sasa awakande vilivyo yaani..[emoji16]
 
Awaase Bangala, Mayele, Djuma, Joyce wajikite kwenye mazoezi... wapunguze muda wanaopoteza saloon.
 
Kashaenda kutia nuksi mpuuzi huyu. Walimruhusuje?
Unajua athari ya kumzuia Raisi wa TFF kwenye issue ya mpira?viongozi wako sio mazuzu kumruhusu.Karia atazuiliwa kuingia nyumbani Kwa manara sio Kambi ya team yoyote ya mpira wa miguu au uwanjani kikiwa kinapigwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…