Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amteua Waziri wa Ulinzi Sebastien Lecomu kuwa Waziri Mkuu

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amteua Waziri wa Ulinzi Sebastien Lecomu kuwa Waziri Mkuu

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemteua waziri wa ulinzi, Sébastien Lecornu, kuwa Waziri Mkuu mpya, akimkabidhi jukumu gumu la kutafuta muafaka katika bunge lililogawanyika na kusimamia kupitishwa kwa bajeti ya mwaka 2026. Hatua hii imekuja baada ya aliyekuwa waziri Mkuu wa nchi hiyo, François Bayrou kuwasilisha rasmi barua ya kujiuzulu Sptemba 8, 2025, ambayo Macron aliikubali.

Bayrou, aliyedumu madarakani kwa miezi tisa pekee, alilazimika kuondoka kutokana na kushindwa kutimiza ahadi yake kuu ya kisiasa kusukuma mbele mpango usiopendwa wa kudhibiti nakisi kubwa ya bajeti ya taifa. Kabla ya kura ya kutokuwa na imani naye, aliwaonya wabunge kuwa kumng’oa hakutafuta suluhisho la matatizo ya nchi na akisisitiza kuwa gharama zinaendelea kuongezeka na deni linaendelea kuwa zito na ghali zaidi

Kwa sasa Waziri Mkuu mpya Sebastien Lecornu anakabiliwa na changamoto mbili kubwa: kuiongoza Ufaransa kutoka kwenye matatizo yake ya kifedha huku akitarajia upinzani mkali wa wananchi. Maandamano ya kitaifa na vizuizi vya barabarani yamepangwa kuanza Jumatano, yakifuatiwa na mgomo mpana wa vyama vya wafanyakazi tarehe 18 Septemba

1757488834924.png

-----------

Beleaguered President Emmanuel Macron has appointed outgoing defense minister Sébastien Lecornu as prime minister, handing him the daunting task of trying to find consensus in a divided parliament and pass the 2026 budget

Earlier on Monday, outgoing Prime Minister François Bayrou submitted his resignation, which Macron accepted. He was forced out after just nine months in office, undone by his failure to deliver a central promise: pushing through an unpopular plan to tame France’s ballooning deficit

Before the confidence vote, Bayrou warned lawmakers that ousting him would not resolve the country’s problems. “You have the power to bring down the government, but you do not have the power to erase reality,” he said. “Reality will remain relentless: expenses will continue to rise, and the burden of debt, already unbearable, will grow heavier and more costly.”

Lecornu now faces the dual challenge of steering France out of its financial morass while leading a government braced for mass protests. Nationwide demonstrations and highway blockades are set for Wednesday, followed by a broader union led strike on September 18


Source: CNN
 
Back
Top Bottom