Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akubali kuipa Marekani madini yake adimu ili iendelee kupata ulinzi

Umesoma umeelewa kweli? Au ni chuki uliyokuwa nayo kwa Zelensky/upendo uliokuwa nao kwa Putin?
Mkuu sasa hapo nani hajaelewa kati yako na huyo jamaa?
Kabla ya Urusi kuivamia Ukraine Urusi ilitaka Ukraine na Marekani kuleta hakikisho la kisheria kuwa Ukraine haitajiunga na Nato lakini Urusi ikajibiwa majibu ya kejeli na dharau.

Mwisho wa siku Urusi imeivamia imechukua 20% ya ardhi, wamechukua %50 ya madini yote, asilimia 40 ya viwanda vyote na bado alicho alicho bakiza na chenyewe kimekuja kuchukuliwa na Marekani na bado Nato hatajiunga sasa hapo hiyo vita waliyo pigana ilikuwa na maana gani?

Wangekubali kusaini kutojiunga nato asingepoteza hivyo vyote.
Kiufupi Zelenskyy alicheza karata zake vibaya.
 
Zelensky na Boris Johnson ndo wameifikisha Ukraine hapa ilikofikia,

Johnson kamjaza Zelensky kukataa Dili la amani kule uturuki mwaka 2022,

Sahv Boris Johnson Baada ya kutumbuliwa uwaziri mkuu, Kawa mwandishi WA habari.

Nae anamnanga Zelensky kwenye magazeti
 
Ndugu Zelenskyy amekamatika
 
Baada ya makubaliano haya,

Ukraine tayar imeshasambaratika vipande

1. Eastern Ukraine, maeneo yote yenye viwanda,ardhi yenye rutuba na madini, yote yanaenda Kwa urusi, na keshasema HAYAWEZI KURUDI KAMWE.

2. KULE KYV, Ni makao makuu TU kama Dodoma, hakuna la maana la Kuendeleza uchumi WA nchi

3. KULE west, tayar marekani keshasema madini na mafuta yatakua yake kufidia gharama za vita.

4. Mpakani na Poland, Nae keshaanza kudai kipande chake.

Kiukweli ZELENSKY atalaaniwa na vizazi vyote vya ukraine
 
kenge kama nyie hamuwezi kuyaona makosa ya jambazi Putin aliyevamia taifa la watu ila mnaona makosa ya mwathiriwa aliyevamiwa na anajitahidi kujitetea
 
Wewe ulieelewa fafanua kwamba amesaini ili iweje madini yachukuliwe yakalipe deni la pesa alizopewa na USA huelewi nn hapo??? Au ndio kujizima akili.
Wapi wamesema amesaini madini yachukuliwe yakalipe deni la pesa? Acha mhemuko. Mpaka sasa terms & conditions za makubaliano hayo ambayo bado hayajasainiwa, hazijawekwa wazi. Kasome CNN kutoka link aliyoweka Mechanic.
 

Muigizaji hana lolote. Alifikiri kuongoza ni rahisi kama kuigiza. Mwanzoni alikuwa anarukaruka, eti hakuna kuchukua madini. Trump kamwambia Zele, sikiliza bwana mdogo, hivi unaelewa maana hakuna free lunch. Embu dondoka saini hapa
 
Tanzania hatupo cheap kihivyo kwa ARV tunaweza kabisa kujitengezea hata Ramadhani madabida alikuwa anatengeneza hapo Dar,kiwanda kilifungwa kwa figisu figisu za makundi ya ccm 2015
 
Zelensk hana akili ameitia hasara kubwa ukraine na itawagarimu maisha yao yote. Kumbe hata ulaya kuna wazungu wapumbavu.
 
hata sijui ulinzi gani, yeye anataka ulinzi badala ya kujenga nchi na uchumi? na ulinzi anaousema ni ulinzi dhidi ya urusi. jambo ambalo marekani hajawahi kuiwa mwaminifu kwa mtu. usimwamini marekani hata kama ameapa
Hizi security Guarantees anatakiwa asign na Jirani Yake Mrusi. Bado anarudia makosa yake yale yale ya kumuamini US.

Zelesky unataka kua ka demu
 
alooo ! kumbe kila kitu kipo planned kweli wasemavyo kwamba hakuna cha bure ni hivyo sasa kama wameweza kufanya hivyo kwa mti mbichi habari gani kwa mti mkavu .Kwa sera hizi za Trump mataifa mengi hasa ya ulimwengu wa tatu ya jiandae kwa mnyonyo.
Niliwahi kusema mahala hawa wakubwa wa huu Ulimwengu wanajua kila hatua ya hivi vita vyote vikubwa Ulimwenguni, sasa kaja Trump anawasainisha mikataba halafu mwingine anakuja kuongoza, kwakweli wanajua na wanajipanga kila uchao kwakunyonya kwa tusio na uwezo wa kujiamulia bila hisani.
 
Daah hapa ndio umefika mwisho wa kufikiri kwako..
 
Muigizaji hana lolote. Alifikiri kuongoza ni rahisi kama kuigiza. Mwanzoni alikuwa anarukaruka, eti hakuna kuchukua madini. Trump kamwambia Zele, sikiliza bwana mdogo, hivi unaelewa maana hakuna free lunch. Embu dondoka saini hapa
Zelenskyy sio mwana siasa ni muigizaji ambaye alipata bahati ya kuwa rais hivyo hakuwa na utashi mkubwa wa siasa.
Mwana siasa yeyote mahili huwa ni mtu anaye jua kuchunga mdomo wake ,na kuchangua maneno ya kuongea kulingana na wakati.
Kauli za Zelenskyy zilichangia pakubwa Urusi kuivamia Ukraine.
 
Ww mwenye fikra ndefu tuambie kulikuwa na haja gani ya zere kungangania kujiunga na Nato?
Pia jiulize mzee putin na familia yake yeye ni nani wa kumpangia mzee zelensky na familia yake aishije, ashirikiane na nani na asijiunge nani!!
 
Pia jiulize mzee putin na familia yake yeye ni nani wa kumpangia mzee zelensky na familia yake aishije, ashirikiane na nani na asijiunge nani!!
Wewe ni mchanga sana kwenye mambo haya. Hujui lolote kuhusu mambo ya geopolitics badala yake unaleta story za Buza. Ndio keshampangia sasa, haya bisha.
 
Zelensky na NATO ni wajanja sana, hapo tayari imekula kwa Russia, lengo la Russia ni US asizidi kusogea mpakani kwake ndo maana akapinga sana Ukraine asijiunge NATO ili US asizidi kumzingila, Ukraine kuwa chini ya Ulinzi wa US kimkataba ni kumfanya Russia asithubutu kurusha hata jiwe Ukraine make akakuwa amechokoza walinzi😄😄😄, na hawa walinzi wana uhuru wa kuleta dhana zao zozote za ulinzi hapo kwenye lindo lao, hapo moja kwa moja NATO iko imezidi kujitanua hadi Ukraine, US ndo NATO.
 
Wewe ni mchanga sana kwenye mambo haya. Hujui lolote kuhusu mambo ya geopolitics badala yake unaleta story za Buza. Ndio keshampangia sasa, haya bisha.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 ndo zenu hizo, blah blah tu, jibu nilichouliza, kuleta blah blah tu hapa bila jibu ni ishara ya umbumbumbu wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…