Habari kutoka Shirika la habari la Reuters zinaeleza kwamba Jasusi mbobezi, Rais wa Urusi, Vladimir Putin alinusirika Kuuawa mwanzoni kabisa mwa mgogoro wa Vita ya Ukraine.
Kwa sasa Putin inawezekana ndiye Rais anayeishi kwa wasiwasi mkubwa kuliko Marais wote wa nchi nyingine duniani.
Putin kwa sasa ni kama anapambania uhai wake, inawezekana maisha yake yapo hatarini kuliko hata ya Zelensky au kiongozi mwingine yeyote yule wa Kremlin.
______________
Vladimir Putin: Rais wa Urusi 'chupuchupu' kuuawa
Rais wa Urusi Vladimir Putin alinusurika katika jaribio la mauaji muda mfupi baada ya kuanza kwa vita nchini Ukraine, afisa mkuu wa jeshi la Ukraine amesema. Baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa, vikiwemo NDTV na New York Post, vimeripoti habari hiyo leo, vikilinukuu gazeti la Ukraine la Ukrainska Pravda.
Jenerali Kyrylo Budanov, mkuu wa upelelezi wa ulinzi wa Ukraine, amefichua habari kuhusu jaribio la kumuua Putin ambalo halikufaulu. Alisema tukio hilo lilitokea katika eneo la Caucasus.
Habari hizo zinakuja huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kati ya Urusi na Ukraine, pamoja na kuongezeka kwa uvumi kuhusu afya ya Putin. Eneo la Caucasus, ambako lilifanyika jaribio la kumuua Putin muda mfupi baada ya kuzuka kwa uhasama nchini Ukraine mnamo Februari 24, liko kati ya Bahari Nyeusi na Bahari ya Caspian.
Taarifa gani hasa zilitolewa na afisa huyu wa upelelezi?
Jenerali Kyrylo Budanov alizungumzia suala hilo katika mahojiano na gazeti la mtandaoni la Ukrainska Pravda.
"Kulikuwa na jaribio la kumuua Putin ... kulingana na maajenti wa Caucasus, si muda mrefu sana uliopita," Bw Budanov alinukuliwa akisema na gazeti la Ukraine.
"Habari hizi hazikuwekwa wazi. Ilikuwa ni kitendo kilichoshindwa kabisa, lakini jaribio hilo lilifanyika kweli ... Ilikuwa takriban miezi miwili iliyopita," aliongeza.
Madai hayo bado hayajathibitishwa na vyanzo huru, lakini habari hizo zinakuja wiki chache baada ya ripoti kuibuka kuwa Bw Putin alifanyiwa upasuaji wa kutoa mafuta kwenye tumbo lake.
Operesheni hiyo "ilifanikiwa sana na hakukuwa na athari", kulingana na ripoti hiyo. Taarifa kuhusu upasuaji wa Putin zilichapishwa kwenye kituo cha Telegram cha SVR, ambacho kinashirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi.
Kulikuwa na taarifa nyingine kutoka kwa mfanyabiashara tajiri ambaye ni rafiki wa karibu wa Putin, ambaye alisema kuwa "Putin anaumwa sana na saratani ya damu".
Mapema mwezi huu, Bw Budanov, katika mahojiano na Sky News, alisema vita vya Ukraine vitakuwa na awamu mpya katikati ya Agosti na vitamalizika mwishoni mwa mwaka, na kusababisha mabadiliko ya utawala nchini Urusi.
Pia alisema kuwa "mapinduzi ya kijeshi" yalikuwa yanaendelea na kwamba hii haiwezi kusitishwa.
Chanzo: BBC