Hashim Thaçi, Rais wa zamani wa Kosovo, amepatikana na hatia ya uhalifu wa kivita ikiwemo mauaji, mateso na kuwashikilia watu kinyume cha sheria na Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ya Kosovo iliyopo The Hague.
Thaçi, mwenye umri wa miaka 58, amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa uhalifu uliodaiwa kufanyika wakati akiwa kamanda mkuu wa Kosovo Liberation Army (KLA) wakati wa mapigano ya Kosovo dhidi ya Serbia katika miaka ya 1990. Mahakama imesema Thaçi alihusika katika mauaji ya watu 96 waliokuwa wapinzani wa kisiasa au waliotuhumiwa kushirikiana na vikosi vya usalama vya Serbia.
Aidha, ametiwa hatiani kwa kuwashikilia watu 385 kinyume cha sheria, kuwatesa watu 303 na kuwafanyia ukatili watu 49. Mahakama imesema waathirika hao hawakuwa wanashiriki katika mapigano wakati uhalifu huo ulipotendeka.
Mahakama imesema Thaçi alishiriki kikamilifu na kuhamasisha uhalifu huo kama sehemu ya mpango wa pamoja wa uhalifu. Waendesha mashtaka walikuwa wameomba ahukumiwe kifungo cha miaka 45 pamoja na makamanda wengine watatu wa zamani wa KLA.
Hata hivyo, jopo la majaji watatu liliondoa mashtaka sita ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, likisema upande wa mashtaka haukuweza kuthibitisha kuwa uhalifu huo ulifanyika katika mfumo wa mashambulizi yaliyoenea au ya kimfumo dhidi ya raia kwa ujumla. Mawakili wa Thaçi walipinga mashtaka hayo wakisema hayakuwa na msingi na yalilenga kubadili historia.
Mahakama hiyo yenye makao yake The Hague, Kosovo Specialist Chambers, ilianzishwa mwaka 2015 kutokana na shinikizo la kimataifa ili kuwafikisha mahakamani wapiganaji wa zamani wa KLA kwa tuhuma za uhalifu uliofanyika wakati na baada ya vita.
Source: Reuters, Le Monde & CNN