Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela endapo mahakama ya Paris itamkuta na hatia ya kutumia kificho fedha kutoka serikali ya aliyekuwa dikteta wa Libya, Muammar Gadhafi, kufadhili kampeni yake ya urais mwaka 2007
Uamuzi wa kesi hiyo unatarajiwa kutolewa Septemba 25, 2025, na endapo atapatikana na hatia, Sarkozy mwenye umri wa miaka 70 atakuwa rais wa kwanza wa zamani wa Ufaransa kutiwa hatiani kwa kupokea fedha haramu kutoka nje ili kushinda uchaguzi
Sarkozy, aliyechaguliwa mwaka 2007 na kushindwa katika jaribio lake la kurejea madarakani mwaka 2012, amekanusha tuhuma hizo zote wakati wa kesi yake ya miezi mitatu mapema mwaka huu 2025. Kesi hiyo pia iliwahusisha washitakiwa wengine 11, wakiwemo mawaziri watatu wa zamani
Licha ya kashfa nyingi za kisheria zilizochafua urithi wake kisiasa, Sarkozy bado ana ushawishi mkubwa katika siasa za mrengo wa kulia nchini Ufaransa na pia kwenye ulimwengu wa burudani kupitia ndoa yake na mwanamuziki na mwanamitindo, Carla Bruni-Sarkozy
Iwapo atapatikana na hatia, anaweza kukata rufaa, hatua ambayo itasitisha utekelezaji wa hukumu hadi rufaa hiyo isikilizwe. Waendesha mashtaka wamependekeza kifungo cha miaka saba jela
Tuhuma hizi ziliibuka mwaka 2011 baada ya shirika la habari la Libya na Gadhafi mwenyewe kudai kuwa serikali ya Libya ilimpa Sarkozy mamilioni ya euro kwa siri ili kufanikisha ushindi wake wa urais mwaka 2007
========
Former French President Nicolas Sarkozy faces up to 10 years in prison if a Paris court convicts him of secretly using funds from the Libyan government of late dictator Moammar Gadhafi to finance his presidential campaign in 2007
The verdict is expected on Thursday. If convicted, the 70-year-old Sarkozy would be the first former French president found guilty of accepting illegal foreign funds to win office
Sarkozy, who was elected in 2007 but lost his bid for reelection in 2012, has denied all wrongdoing during a three-month trial earlier this year that also involved 11 co-defendants, including three former ministers
Despite multiple legal scandals that have clouded his presidential legacy, Sarkozy remains an influential figure in right-wing politics in France and in entertainment circles, by virtue of his marriage to singer and model Carla Bruni-Sarkozy
Sarkozy can appeal a guilty verdict, which would suspend the sentence pending the appeal. Prosecutors have argued for a seven-year prison sentence
The accusations trace their roots to 2011, when a Libyan news agency and Gadhafi himself said that the Libyan state had secretly funneled millions of euros into Sarkozy's 2007 campaign
Source: African news