SI KWELI Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema atangaza kutogombea muhula wa pili uchaguzi Mkuu mwaka 2026

SI KWELI Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema atangaza kutogombea muhula wa pili uchaguzi Mkuu mwaka 2026

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Licha ya kufanya makubwa kwa muda mfupi ndani ya Mhula wa Kwanza, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ametangaza hataomba muhula wa pili kwenye uchaguzi mkuu wa baadae 2026.

imageresize.jpg

Hapa Tanzania hakuna chochote kafanya na bado chawa wanataka aongeze muda mpka 2030!

Tamaa na Uroho wa Madaraka. Tazama video hii ujionee mwenyewe.



Video ya Rais Hakainde Hichilema akisema hatagombea tena mwaka 2026.
 
Tunachokijua
Oktoba 15, 2023, Mtumiaji wa Mtandao wa X anayefahamika kwa jina la Gasper E. Temba, PVR alichapisha ujumbe unaodokeza sehemu ya hotuba ya Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akidokeza kuwa hatagombea tena kwa muhula wa pili kwenye uchaguzi wa mwaka 2026.

photo_2023-10-16_13-39-45-jpg.2783664

Picha yenye ujumbe kutoka mtandao wa X
Chapisho hilo lilifutwa masaa kadhaa baadae, hata hivyo, hadi linafutwa tayari lilikuwa limesomwa mara 1363, watu 10 walishirikisha wengine na zaidi ya wachangiaji 10 walitoa maoni yao.

Hakainde Hichilema ni nani hasa?
Hakainde Hichilema alizaliwa Juni 4, 1962, ni mfanyabiashara, mkulima, na mwanasiasa wa Zambia ambaye ni Rais wa sasa wa Zambia tangu Agosti 24, 2021.

Baada ya kugombea chaguzi tano za mwaka 2006, 2008, 2011, 2015 na 2016, alishinda uchaguzi wa urais wa 2021 kwa 59.02% ya kura na ameongoza chama cha United Party for National Development tangu 2006 kufuatia kifo cha mwanzilishi wa chama Anderson Mazoka.

Kabla ya kuchaguliwa kwake, Hichilema alikuwa mpinzani mkubwa wa Edgar Lungu, Rais wa Zambia kutoka 2015 hadi 2021. Mnamo Aprili 11, 2017, Hichilema alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini, hatua ambayo ilionekana kama kitendo kisicho halali na Lungu kunyamazisha mpinzani wa kisiasa.

Kukamatwa na kushtakiwa kulilaaniwa pakubwa, huku maandamano yakifanyika nchini Zambia na nje ya nchi, yakitaka Hichilema aachiliwe na kulaani kuongezeka kwa ubabe wa utawala wa Lungu.

Hichilema aliachiliwa kutoka gerezani, Agosti 16, 2017, na shtaka la uhaini likatupiliwa mbali.

Kutokugombea mwaka 2026
Kama ilivyobainishwa awali, video yenye chapisho la kauli hii lilitolewa kwenye mtandao wa X Oktoba 15, 2023.

"Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa changamoto ambazo tumekumbana nazo wakati wa uongozi wangu kama kiongozi wa taifa hili. Ni kwa dhati kabisa na kwa hisia kubwa ya uwajibikaji kwa taifa letu ambapo natangaza uamuzi wangu wa kutogombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao wa 2026.

Ninaamini uamuzi huu ni kwa maslahi ya nchi yetu na mustakabali wake.”
Ni sehemu ya maneno yanayotamkwa kwenye video hiyo.

JamiiForums imefuatilia undani wa video hii yenye sekunde 55 na kubaini kuwa ilipostiwa kwa mara ya kwanza Septemba 22, 2023 kwenye mtandao wa TikTok na mtumiaji aliye jisajili kwa jina la Zambian AI.

Aidha, katika kufuatilia ukweli wa madai haya, JamiiForums imebaini kuwa video hii imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili bandia (AI).

Baadhi ya mambo yanayoweza kubabainisha uhalisia wake ni kivuli kilichopo kwenye koti na uwiano wa kuchwa na shingo.

Ufutiliaji wa akaunti ya mhusika umebainisha kuwa hii sio video ya kwanza kuitengeneza kwa mfumo huu.

Video zingine zilizopo zinamhusisha Rais wa zamani wa taifa hilo Edgar Lungu ambazo pia zimetengenezwa kwa teknolojia ya akili bandia.

Hivyo, JamiiForums imejiridhisha pasipo shaka kuwa video hizo siyo halisi, na Rais Hichilema hajazungumza popote kutokugombea tena mwaka 2026 kama inavyodaiwa kwenye video husika.
Back
Top Bottom