Uchaguzi 2020 Rais wa Zanzibar 2020 aweje?

battawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Posts
2,712
Reaction score
2,577
Heri za Siku kuu ya Eid na Baraka tele za Mfungo wa Ramadhan. Poleni kwa kupambana na maisha na Ugonjwa thikili wa Corona.

Sasa wakati wa kufuma viongozi watakao iongoza ama kuitawla nchi zetu mbili ndani ya Jamuhuri ya Muungano umefika.

Ila jioni ya leo nitajihusisha upandewa Zanzibar. na uchaguzi ujao. Wote tunayakumbuka yaliyotokea 2015 pale Jecha alipokuwa kinara wa sarakasi za result za uchaguzi na kisha kufuta uchaguzi uiokuwa huru na haki bila ya hata fujo wakati wa upigaji kura na waakati wa kutowa matokeo. Bali fujo aliiunda yeye Muheshimiwa kwa kusema kuna kituo kimoja Pemba eti kilizidisha idadi ya kura zaidi ya waliopiga. Hapo akapata uhalali wa kufuta uchaguzi wote.

Hata hivyo, Miaka mitano imekwisha, wengi wameshakubaliana na matokeo na wanajipanga na yajayo.
Hivi sasa gumzo Mitaani limeanza kutanada kuzungumzia ni nani atakuwa Mteuliwa wa vyama vya siasa kugombea nafasi ya Urais Zanzibar 2020.

CCM wakiwataja Mama samia, Husein mwinyi, Makame Mbarawa, Ali karume...

Wakati ACT Wazalendo kikiwa ni chama kinachotarajiwa kuleta upinzani mkubwa mwaka huu ZNZ na sio tena CUF kama ilivyozoweleka huko nyuma.

Kuna tetesi kuwa, Maalim Seif, Mansour Yussuf Himid, Mazrui, Babu Juma Duni, na wengine wanadhani aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ambaye alifukuzawa kazi wakati wa bunge la katiba Bw.Othman Masoud.

Wote tunajuwa kuwa CCM inapwagia maji huku Zanzibar, kwani kila uchaguzi huambulia bao la Mkono. Hupanga na kupangua kuweka mikakati na mbinu za kupata ushindi mtakatifu, lakini huishia kulamba mchanga na Kuanza figisu za kimkakati.

Si jui kwa nini hujihangaisha kiasi kikubwa hiki wakati wakijuwa fika kuwa Hata wakishindwa ,bado washindi ni wao.

Nadhani wanajaribu kutafuta uchochoro wa kuhalalisha iliyo haramu kwenye meza ya kura, jambo ambalo si rahisi kiivyo pale unaposhindana na binadamu mweledi kama wewe tena kipenzi cha wengi.

Yote hayo si shani, Shani ni kumpata Rais awe wa chama chochote kile ambaye Atatuwekea vipa umbele vinavyo kubalika.

Zanzibar kuna Hoja nzito ya kuona Muungano ni kikwazo cha ustawi wa Zanzibar kam nchi na kuna kila dhamira na nia ya kujinasua na mkwamo huu. Kudhamiria kuchimba mafuta, Kuanzisha uvuvi wa bahari kuu, Kujenga Bandari kubwa na ya Kisasa, Kujenga viwanda vikubwa kama kile cha Maziwa na Sukari ambavyo bidhaa zake zitaingia kwenye soko la Tanzania na Afrika Mashariki. Lakini Vikwazo vikubwa kwa nduguzetu wa damu vimekwamisha juhudi hizi. Utadhani serikali ya Zanzibar si ya CCM ileile ya Bara. Kwenye uchumi, wenzetu hawana cha Muungano.

Kwa hiyo Raisi ajaye ayajuwe haya yafuatayo ikiwa ni vipaumbele vya Wazanzibari wote bila ya kujali vyama vyao:

Atuahidi yafuatayo:
  1. Awe Mzalendo Mzanzibari mwenye kuipenda, kuitetea na kuilinda Dola ya Zanzibar na Maslahi yake ndani ya Muungano.​
  2. Asiwe Mbaguzi kwa wazanzibari wenye asili tofauti tofauti (Wahindi, Watanganyika, Waoman, Wachina,wasomali, Wayemen, Wazungu na Wangazija.​
  3. Asimamie ajenda ya Mamlaka kamili na Muungano wenye usawa kwa Pande zote.
  4. Adumishe udugu wetuwa damu na Oman, Tanganyika, China, India, Yemen, Somalia, Indonesia na Commoro ambazo zote nchi hizo zina muingiliano mkubwa na Zanzibar tangu zama na zama.​
  5. Atuahidi kutupatia katiba mpya itakayoharamisha ubaguzi wa aina yoyote na kuwa kosa la jinai kwa mwenye kuusema, kuutangaza au kuutetea ubaguzi wa kijinsia, kikabila, (kama wele wanaowachukia machotara) na kimadhehebu​
  6. Alete mtengamano wa kitaifa (Commission of truth and reconciliation) utakao ruhusu kila mwenye makovu ya uovu aliofanyiwa na chombo chochote kiwe cha dola au mtu binafsi tokea Mapinduzi hadi leo aje hadharani mbele ya tume aueleze na kuridhiana, kusameheana au kupeleka kesi yake mahakamani.​
  7. Atuahidi Tume huru ya uchaguzi, mahakama huru, na Uhuru wa kujieleza bila ya vikwazo kwa kila raia na kulindwa haki za kila raia wa Zanzibar na hakizake zipewe kipaumbele dhidi ya raia wa nchi yoyote duniani. Kama ilivyo nchi za wenzetu Arabuni, au India, au UK.​
  8. Aimarishe Serikli ya Umoja wa kitaifa na kuiheshimu mfumo wake.​
NB: Ifahamike kuwa​

Mgombea Urais yoyote yule awe wa chama chochote kile akituahidi kutuchimbia mafuta ama gesi au kujenga viwanda vya samaki bila ya kubadili mfumo wa siasa (Muundo wa Muungano) huyo anatudanganya, kama walivyotudanganya watangulizi wake.

Nashauri Tusimuunge mkono, ni heri tubaki bila kupiga kura ikiwa wote watakuwa na muelekeo huo wa kutudanganya.

HII NDIO ZANZIBAR TUITAKAYO KWA RAISI AJAYE LAZIMA AJIPANGE HIVYO

Nawasilisha

 
Huyu Mwanasheria Mkuu mdtaafu Othman Masoud kwa hakika ni "presidential material". Ni muda sahihi kwa Maalim Seif kumuamini na hata kumpisha apeperushe bendera kwa nafasi ya uraisi ktk chama chake.
 
Huyu Mwanasheria Mkuu mdtaafu Othman Masoud kwa hakika ni "presidential material". Ni muda sahihi kwa Maalim Seif kumuamini na hata kumpisha apeperushe bendera kwa nafasi ya uraisi ktk chama chake.
Upo sahihi kwa misingi kushiba itikadi na independent decision yule jamaa Ni noma.
Alipoteza kazi kwa kuonesha yeye Ni mwenye msimamo usioyumba
 
1. Atoke Bara
2. Awe mkristo
3. Atoke chama cha upinzani kama CHADEMA, n.k
 
1. Atoke Bara
2. Awe mkristo
3. Atoke chama cha upinzani kama CHADEMA, n.k
Ki vipi?
Akitoka bara hawezi kutimiz mashariti ya kuwa raisi wa ZNZ
Kuwa mkiristo si hoja, alimradi awe Mzanzibari. Wapo akina Castiko hapa zenji na Mwakanjuki, au Akina Dourado ambao waliwahi kuwa Mwanasheria mkuu wa SMZ mara baada ya Mapinduzi.
Kuhusu Chadema, ikiwa tutaunda Ukawa na wakaleta mgombea mwenye ushawishi ,hakuna shida endapo ACT au CCM watamkubali kuwa mgombea wao.
 
Fatma Karume as an Independent candidate atakuwa rais mimi hapa nitamuoa hivi karibuni.
 
Ni vizuri na mtu kutoka Bara akawa rais Zanzibar kama ambavyo mtu kutoka Zanzibar aliwahi kuwa rais Bara. Pia ni vizuri hata mawaziri wa Zanzibar na wakuu wa mikoa na wilaya n.k. baadhi wakatoka Bara.

Pia ni vizuri kama mkristo akawa rais wa Zanzibar ili kutoa fursa kwa dini zote kwani Zanzibar pia kuna wakristo na haikuwahi kutokea Zanzibar wakawa na rais mkristo tangu mapinduzi.

Pia ni wakati wa Zanzibar na Bara pia kubadilisha chama manake ccm ipo tangu mwaka 1954 ni zaidi ya miaka 60 sasa.
 
#Katiba mpya... Katiba mpya... Katiba ya mwananchi... serikali tatu...
 
Sasa tumesha wapata wagombea wa kila chama
Zanzibar na Bara
Nakumbushia tena vipaumbele hivi kwa Risi tumtakae zanzibar sisi wananchi tuna matakwa yetu atuahidi kuyasimamia ili tumpe kura na ridhaa ya kutuongoza.
Atuahidi yafuatayo:
  1. Aimarishe Serikli ya Umoja wa kitaifa na kuiheshimu mfumo wake.

  2. Awe Mzalendo Mzanzibari mwenye kuipenda, kuitetea na kuilinda Dola ya Zanzibar na Maslahi yake ndani ya Muungano.
  3. Asiwe Mbaguzi kwa wazanzibari wenye asili tofauti tofauti (Wahindi, Watanganyika, Waoman, Wachina,wasomali, Wayemen, Wazungu na Wangazija.
  4. Asimamie ajenda ya Mamlaka kamili na Muungano wenye usawa kwa Pande zote.
  5. Adumishe udugu wetu wa damu na Oman, Tanganyika, China, India, Yemen, Somalia, Indonesia na Commoro ambazo zote nchi hizo zina muingiliano mkubwa na Zanzibar tangu zama na zama.
  6. Atuahidi kutupatia katiba mpya itakayoharamisha ubaguzi wa aina yoyote na kuwa kosa la jinai kwa mwenye kuusema, kuutangaza au kuutetea ubaguzi wa kijinsia, kikabila, (kama wele wanaowachukia machotara) na kimadhehebu
  7. Alete mtengamano wa kitaifa (Commission of truth and reconciliation) utakao ruhusu kila mwenye makovu ya uovu aliofanyiwa na chombo chochote kiwe cha dola au mtu binafsi tokea Mapinduzi hadi leo aje hadharani mbele ya tume aueleze na kuridhiana, kusameheana au kupeleka kesi yake mahakamani.
  8. Atuahidi Tume huru ya uchaguzi, mahakama huru, na Uhuru wa kujieleza bila ya vikwazo kwa kila raia na kulindwa haki za kila raia wa Zanzibar na hakizake zipewe kipaumbele dhidi ya raia wa nchi yoyote duniani. Kama ilivyo nchi za wenzetu Arabuni, au India, au UK. NB: Ifahamike kuwa Mgombea Urais yoyote yule awe wa chama chochote kile akituahidi kutuchimbia mafuta ama gesi au kujenga viwanda vya samaki bila ya kubadili mfumo wa siasa (Muundo wa Muungano) huyo anatudanganya, kama walivyotudanganya watangulizi wake.


    Nashauri Tusimuunge mkono, ni heri tubaki bila kupiga kura ikiwa wote watakuwa na muelekeo huo wa kutudanganya.

HII NDIO ZANZIBAR TUITAKAYO KWA RAISI AJAYE LAZIMA AJIPANGE HIVYO

Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…