battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,712
- 2,577
Heri za Siku kuu ya Eid na Baraka tele za Mfungo wa Ramadhan. Poleni kwa kupambana na maisha na Ugonjwa thikili wa Corona.
Sasa wakati wa kufuma viongozi watakao iongoza ama kuitawla nchi zetu mbili ndani ya Jamuhuri ya Muungano umefika.
Ila jioni ya leo nitajihusisha upandewa Zanzibar. na uchaguzi ujao. Wote tunayakumbuka yaliyotokea 2015 pale Jecha alipokuwa kinara wa sarakasi za result za uchaguzi na kisha kufuta uchaguzi uiokuwa huru na haki bila ya hata fujo wakati wa upigaji kura na waakati wa kutowa matokeo. Bali fujo aliiunda yeye Muheshimiwa kwa kusema kuna kituo kimoja Pemba eti kilizidisha idadi ya kura zaidi ya waliopiga. Hapo akapata uhalali wa kufuta uchaguzi wote.
Hata hivyo, Miaka mitano imekwisha, wengi wameshakubaliana na matokeo na wanajipanga na yajayo.
Hivi sasa gumzo Mitaani limeanza kutanada kuzungumzia ni nani atakuwa Mteuliwa wa vyama vya siasa kugombea nafasi ya Urais Zanzibar 2020.
CCM wakiwataja Mama samia, Husein mwinyi, Makame Mbarawa, Ali karume...
Wakati ACT Wazalendo kikiwa ni chama kinachotarajiwa kuleta upinzani mkubwa mwaka huu ZNZ na sio tena CUF kama ilivyozoweleka huko nyuma.
Kuna tetesi kuwa, Maalim Seif, Mansour Yussuf Himid, Mazrui, Babu Juma Duni, na wengine wanadhani aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ambaye alifukuzawa kazi wakati wa bunge la katiba Bw.Othman Masoud.
Wote tunajuwa kuwa CCM inapwagia maji huku Zanzibar, kwani kila uchaguzi huambulia bao la Mkono. Hupanga na kupangua kuweka mikakati na mbinu za kupata ushindi mtakatifu, lakini huishia kulamba mchanga na Kuanza figisu za kimkakati.
Si jui kwa nini hujihangaisha kiasi kikubwa hiki wakati wakijuwa fika kuwa Hata wakishindwa ,bado washindi ni wao.
Nadhani wanajaribu kutafuta uchochoro wa kuhalalisha iliyo haramu kwenye meza ya kura, jambo ambalo si rahisi kiivyo pale unaposhindana na binadamu mweledi kama wewe tena kipenzi cha wengi.
Yote hayo si shani, Shani ni kumpata Rais awe wa chama chochote kile ambaye Atatuwekea vipa umbele vinavyo kubalika.
Zanzibar kuna Hoja nzito ya kuona Muungano ni kikwazo cha ustawi wa Zanzibar kam nchi na kuna kila dhamira na nia ya kujinasua na mkwamo huu. Kudhamiria kuchimba mafuta, Kuanzisha uvuvi wa bahari kuu, Kujenga Bandari kubwa na ya Kisasa, Kujenga viwanda vikubwa kama kile cha Maziwa na Sukari ambavyo bidhaa zake zitaingia kwenye soko la Tanzania na Afrika Mashariki. Lakini Vikwazo vikubwa kwa nduguzetu wa damu vimekwamisha juhudi hizi. Utadhani serikali ya Zanzibar si ya CCM ileile ya Bara. Kwenye uchumi, wenzetu hawana cha Muungano.
Kwa hiyo Raisi ajaye ayajuwe haya yafuatayo ikiwa ni vipaumbele vya Wazanzibari wote bila ya kujali vyama vyao:
Atuahidi yafuatayo:
Mgombea Urais yoyote yule awe wa chama chochote kile akituahidi kutuchimbia mafuta ama gesi au kujenga viwanda vya samaki bila ya kubadili mfumo wa siasa (Muundo wa Muungano) huyo anatudanganya, kama walivyotudanganya watangulizi wake.
Nashauri Tusimuunge mkono, ni heri tubaki bila kupiga kura ikiwa wote watakuwa na muelekeo huo wa kutudanganya.
HII NDIO ZANZIBAR TUITAKAYO KWA RAISI AJAYE LAZIMA AJIPANGE HIVYO
Nawasilisha

- Awe Mzalendo Mzanzibari mwenye kuipenda, kuitetea na kuilinda Dola ya Zanzibar na Maslahi yake ndani ya Muungano.
- Asiwe Mbaguzi kwa wazanzibari wenye asili tofauti tofauti (Wahindi, Watanganyika, Waoman, Wachina,wasomali, Wayemen, Wazungu na Wangazija.
- Asimamie ajenda ya Mamlaka kamili na Muungano wenye usawa kwa Pande zote.
- Adumishe udugu wetuwa damu na Oman, Tanganyika, China, India, Yemen, Somalia, Indonesia na Commoro ambazo zote nchi hizo zina muingiliano mkubwa na Zanzibar tangu zama na zama.
- Atuahidi kutupatia katiba mpya itakayoharamisha ubaguzi wa aina yoyote na kuwa kosa la jinai kwa mwenye kuusema, kuutangaza au kuutetea ubaguzi wa kijinsia, kikabila, (kama wele wanaowachukia machotara) na kimadhehebu
- Alete mtengamano wa kitaifa (Commission of truth and reconciliation) utakao ruhusu kila mwenye makovu ya uovu aliofanyiwa na chombo chochote kiwe cha dola au mtu binafsi tokea Mapinduzi hadi leo aje hadharani mbele ya tume aueleze na kuridhiana, kusameheana au kupeleka kesi yake mahakamani.
- Atuahidi Tume huru ya uchaguzi, mahakama huru, na Uhuru wa kujieleza bila ya vikwazo kwa kila raia na kulindwa haki za kila raia wa Zanzibar na hakizake zipewe kipaumbele dhidi ya raia wa nchi yoyote duniani. Kama ilivyo nchi za wenzetu Arabuni, au India, au UK.
- Aimarishe Serikli ya Umoja wa kitaifa na kuiheshimu mfumo wake.
NB: Ifahamike kuwa