Rais wa Zanzibar aagiza Meli zote za Serikali ziuzwe kwa vile hazileti faida

Rais wa Zanzibar aagiza Meli zote za Serikali ziuzwe kwa vile hazileti faida

Kuna haja ya kubadili mifumo ya nishati ya meli za serikali. Serikali iangalie uwezekano wa meli zote mpya zinazojengwa ziwa Victoria, Tanganyika na bahari ya Hindi kutumia nishati ya gesi ambayo ni nafuu sana ili meli hizi zianze kuendeshwa kwa faida.
Mwinyi pia angefanya 'last attempt' kwa kutenga fedha na kununua gas fired engines na kufunga kwenye baadhi ya meli, hasa zile ambazo ni mpya-mpya aone kama ufanisi utaongezeka kwa kupugua kwa gharama ya nishati.
Gas is our future...
 
Kuna haja ya kubadili mifumo ya nishati ya meli za serikali. Serikali iangalie uwezekano wa meli zote mpya zinazojengwa ziwa Victoria, Tanganyika na bahari ya Hindi kutumia nishati ya gesi ambayo ni nafuu sana ili meli hizi zianze kuendeshwa kwa faida.
Mwinyi pia angefanya 'last attempt' kwa kutenga fedha na kununua gas fired engine na kufunga kwenye baadhi ya meli, hasa zile ambazo ni mpya-mpya aone kama ufanisi utaongezeka kwa kupugua kwa gharama ya nishati.
Gas is our future...
Kwani Azam nao meli zao wanatumia gesi ?
 
Hussein Mwinyi ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ameagiza meli zote zinazomilikiwa na serikali hiyo ziuzwe kwa vile zinaleta hasara , ameagiza ziuzwe ili WAANZE UPYA .

Cha kushangaza sasa ! serikali ya Muungano yenyewe inaendelea kununua ndege huku zikileta mabilioni ya Hasara hadi kamati ya bunge imepigwa na bumbuwazi ! Je lengo lao ni nini ?
Imetokea nini?

Sifa nyingi tuu alishushiwa Dr Shein na kuwa kiongozi bora.
Lakini kila alipogusa mwinyi kuna uoza mtupu.
Naukweli hausemwi na wale walo sababisha uovu hawatajwi au kushughulikiwa.
Meli ya Mapinduzi II watu walisema sana kuwa ni second hand na sio mpya na nimbovu lakini Viongozi wote walitetea sana.

Wafanya kazi wote hawana ujuzi wakzai . Ni wakindugu. Sasa shirika linakwenda kihasara .
Leo hii kama mtu binafsi atinunuwa ile meli basi itafanya kazi na kutia faida kubwa sana.

Shirika la meli lilipasa kuchaguwa wafanya kazi kwa kutegemea elimu sio uCCM . Likiwa katika hasara manager na wote wengine basi kazi na kushtakiwa.

Leo kimya hakuna hatuwa yoyote inayo chukuliwa.
 
Kwani Azam nao meli zao wanatumia gesi ?
Zile ni boat. Sio meli. Meli unazijua wewe? Meli moja inaweza kuwa na injini mbili kila moja ikizalisha Megawat moja hadi mbili. Na nikiangalia kwenye chati injini ya megawatt moja inatumia galoni 71 za Diesel. Hii ni takribani lita 350 kwa saa kwa injini moja. Kwa meli yenye engine mbili itatumia takriban lita 700 za Diesel kwa saa.
Sasa ukiwa na meli kama Mv Victoria ambayo naasume inazalisha megawatt mbili hii itatumia galon 140 za diesel kwa saa ambayo ni takriban lita 700 kwa saa. Na kwa meli 'inayokaa' kwenye maji kwa masaa 12, you can imagine itumie lita 9,000 za Diesel kwa safari moja. Unapataje faida kirahisi?
Matumizi ya natural gas huweza kupunguza gharama za nishati kwa takrabini asilimia 40 hivyo kupunguza running cost.
Kwa wenzetu wanao endesha yale ma meli makubwa nasikia huwa wanatumia mafuta 'machafu' ambayo ni mazito mithili ya lami na hivyo ndivyo wanavyoweza kupunguza costs.
Screenshot_20210904-013722.jpg
 
Hussein Mwinyi ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ameagiza meli zote zinazomilikiwa na serikali hiyo ziuzwe kwa vile zinaleta hasara , ameagiza ziuzwe ili WAANZE UPYA .

Cha kushangaza sasa ! serikali ya Muungano yenyewe inaendelea kununua ndege huku zikileta mabilioni ya Hasara hadi kamati ya bunge imepigwa na bumbuwazi ! Je lengo lao ni nini ?
Bro Visiwani anajielewa, kama Obama vile!
 
Hata ile meli 'mpya' ya MV Mapinduzi II ya mwaka 2015 tayari ni chakavu bila kusahau meli ya MT Mkombozi II maalum kama tanker ya mafuta muda mwingi imetia nanga bandarini Malindi Zanzibar bila kupiga kazi!.

8 August 2019
MT Ukombozi II meli mpya yatinga Zanzibar

UKOMBOZI II - Tanker (IMO: 9851012, MMSI: 677044600)
The vessel UKOMBOZI II (IMO: 9851012, MMSI: 677044600) is a Tanker It's sailing under the flag of [TZ] Tanzania

MV MAPINDUZI II , meli mpya inayoendelea kukumbwa na changamoto zisizoisha


Je ni ukweli kuwa Hii ndio Posco Plantec meli mbovu, kongwe iliyobadilishwa jina na kuitwa (Mapinduzi II)
Source : Hilmi Hilal
https://www.balticshipping.com › imo
MAPINDUZI II, Passenger vessel, IMO 9708485 - BalticShipping.com
MAPINDUZI II is a Passenger vessel built in 2015. Currently sailing under the flag of Tanzania. Formerly also known as POSCO PLANTEC 13SV01
 
Meli za SMZ ni kuukuu sana hazipati wateja wa kutosha

Meli kadhaa za binafsi ni meli zilizonunuliwa toka kwa waendeshaji wengine zikafanyiwa ukarafati wa hali ya juu zinadunda mzigo pia kuwa na certificate safi kabisa za usalama wa kufanya kazi baharini pia kuendeshwa na manahodha, engineers na mabaria wenye ujuzi wa hali ya juu , tujiulize vipi SMZ wameshindwa kuendesha meli zao brand new toka South Korea na Netherlands?

IMO number9708485
MMSI677015400
Name of the shipMAPINDUZI II
Former namesPOSCO PLANTEC 13SV01 (2015)
Vessel typePassenger vessel
Operating statusActive
FlagTanzania
Gross tonnage5464 tons
Deadweight795 tons
Length90 m
Breadth17 m
 
Watu binafsi wanazidi kutoa huduma nzuri na bora huku kila siku wakileta vyombo vipya

1 September 2021
Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Hussein Mwinyi azindua meli MV Ikraam I (uwezo abiria 1,200 na mizigo tani 400 / magari 32 mchanganyiko). Mmiliki ni kampuni ya (kiTanzania/ Zanzibar) Ikraam Sealine .

Source : KTV TZ ONLINE
The vessel IKRAAM I (IMO: 9848962, MMSI 677014300) is a Passenger/Ro-Ro Cargo Ship built in 2018 (3 years old) and currently sailing under the flag of Tanzania.
1630711594934.png
 
Ma-CCM ni failure kwenye kila kitu.

Watauza halafu wakinunua watarudi tena kulele maana hakuna mipango wala kujipanga bali wanasiasa ndio wanaamua kila kitu huku wataalamu wakibaki kuwa watekelezaji.

Na kwenye huu ununuzi, kunaweza pia kukawa na agenda ya upigaji.

Sina imani naa hawa watu.
 
Hivi kwanini serikali huwa inafeli kwenye biashara nini tatizo haswa?

Ule uchungu na ile biashara watendaji hawana jiulize mtu binafsi amudu kuendesha chombo chake chombo cha wengi ishindikane
 
Back
Top Bottom