Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi anatangaza Baraza jipya la Mawaziri. Hakuna Manaibu Waziri

Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi anatangaza Baraza jipya la Mawaziri. Hakuna Manaibu Waziri

Rais wa Zanzibar Dr Hussein Mwinyi yupo mubashara Channel ten anatangaza baraza jipya la mawaziri..
Nimependa majina yao kuwa yenye asili moja, hakuna jina lenye asili ya mabeberu! Labda kwa mbali Riziki na Tabia
 
Ntawashangaa sana ACT kama wakikubali kuingizwa kwenye hilo baraza
 
sasa wote hao wa nini wakati nchi yenyewe kama mkoa moja tu wa bara, si aendeshes nchi nzima peke yake tu kama mkuu wa mkoa. Ni kupoteza hela za umma tu.
 
Ila kweli,zanzibar naibu waziri wa nini.

Hata hao wawakilishi ni wengi sana aisee.

Ilikuwa zanzibar wawakilishi wachache wanatosha,sehemu ndogo sana hii.

Yani nchi ambayo ukubwa wake ni kama mkoa wa lindi ati ina wawakilishi kibaoo.

Nchi ambayo watu wake idadi ni ndogo kuliko idadi ya watu wa daresalam ati ina wawakilishi kibaoooo
Una ufahamu wa ukubwa wa mkoa wa Lindi?
Eneo la mkoa wa Lindi lina Ukubwa: 66,040 km²

Zanzibar (Unguja na Pemba na visiwa vyote) ina ukubwa wa eneo la
2,462 km2

Nikueleze tu Lindi ni kubwa mara 26.8

Kwa lugha rahisi kwa wasiojua hesabu ni kuwa kuna Zanzibar 26 ndani ya Mkoa wa Lindi.
Zanzibar yote ni kama mara mbili ya mkoa wa Dar es Salaam yenye ukubwa wa kilometa za mraba 1,393.
 
Mkuu nisamehe bure pengine nilikosea kuwasilisha mada kutokana na ufinyu wa taarifa.

Lakini ambacho nilikusudia ni kuwa zanzibar ni kama lindi tu kwa maana ile ya kuwa zanzibar haiizidi lindi ukubwa.

Kwa kqeli mambo ya kilomita za mraba umenipa utaalamu.

Naomba niedit pale ili kuweka sawa zaidi taarifa
 
Nisamehe pia kama nimewasilisha kwa mbwembwe.
Sisi watu wa takwimu huwa tuna wasilisha kwa namna hiyo.
Tupo pamoja mkuu.
Siku njema.
 
Rais wa Zanzibar Dr Hussein Mwinyi yupo mubashara Channel ten anatangaza baraza jipya la mawaziri.

Baraza la mawaziri limetangazwa lakini Wizara mbili zimebaki wazi na uteuzi utafanywa baadae nazo ni Wizara ya afya na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Rais Mwinyi amesema kwa sasa hakutakuwa na Manaibu Waziri na endapo siku za mbele itajitokeza wizara itakayoonyesha umuhimu wa kuwepo naibu waziri basi atateuliwa.

Kuhusu wizara mbili kuwa wazi ni kwamba ACT wazalendo hawajapeleka majina kwa mujibu wa katiba na wala wawakilishi wake hawajala viapo hivyo wanasubiriwa.

========

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI ZANZIBAR:

1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji - Mudrik Ramadhan Soraga.

2. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) - Masoud Ali Mohammed.

3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora - Haroun Ali Suleiman.

4. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango - Jamal Kassim Ali.

5. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi - Dokta Khalid Mohammed Salum.

6. Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo - Soud Nahoda Hassan.

7. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali - Simai Mohammed Said

8. Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni - Tabia Mwita Maulid.

9. Wizara ya Biashara ya Maendeleo ya Viwanda. Hakuna Waziri.

10. Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi - Riziki Pembe Juma.

11. Wizara ya Maji na Nishati - Suleiman Masoud Makame.

12. Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto. Hakuna Waziri.

13. Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale - Lela Mohammed Mussa.

14. Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi - Abdallah Hussein Kombo.

15. Wizara ya Ujenzi - Rahma Kassim Ali.
Hivi huko ni kweli Hakuna Mkristo hata mmoja? [emoji53]
 
Zanzibar kuna kadhi mkuu!

Hahahaha kule bwashee hadi kuna gwaride anakagua Amir wa Vikosi katika sikukuu ya kidini. Gwaride la Eid FFU wanavaa nadhifu kabisa na kofia zao za vinyoya.

Wengi wape. Ni haki yao
 
Back
Top Bottom