Rais wa Zanzibar kuwa mbadala wa makamu wa Rais katika kumuwakilisha Rais wa Tanzania katika baadhi ya mikutano ni sawa?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Tumeshazoea Rais wetu akibanwa anampeleka Mwinyi kumuwakilisha katika shughuli na vikao vya nje ya nchi,

Mfano leo Dk. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar kuelekea nchini Qatar kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kimataifa la tatu la uchumi linalofanyika Jijini Doha. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya Washiriki ikiwa ni pamoja na Viongozi wa kampuni kubwa duniani na Viongozi wa juu wa Serikali.

Phillip Mpango hayupo, kawekwa kuwa pambo au?
 
Sisi wote ni ndugu 🎶🎶🎶🎵🎵🎵🎶🎶🎶🎶
Watoto wa baba mmoja🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎶🎵🎵🎵🎵🎵🎵
 
Rais ana Mamlaka ya kumteua yeyote kumuwakilisha kwny kikao

alishamteua Awesu Waziri wake wa Maji kwny Hadhara kuu ya Maji Mjini New York hivi karibuni, kishamteua Waziri Gwajima kumuwakilisha katika Mkutano Mkuu wa masuala ya jinsia hata Mstaafu Jk kishamwakilisha sio tu Mh.Samia bali hata Hayati JPM

Dr.Mpango nae pia kishamwakilisha Rais kwny vikao vingi vya nje

Rais Samia moja ya sifa yake kubwa inayomtofautisha na Watangulizi wake ni kutokukurupuka kwny maamuzi
 
Tumeshazoea Rais wetu akibanwa anampeleka Mwinyi kumuwakilisha katika shughuli na vikao vya nje ya nchi,

Mfano leo Dk. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar kuelekea nchini Qatar kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kimataifa la tatu la uchumi linalofanyika Jijini Doha. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya Washiriki ikiwa ni pamoja na Viongozi wa kampuni kubwa duniani na Viongozi wa juu wa Serikali.

Phillip Mpango hayupo, kawekwa kuwa pambo au?
WaZanzibar wametupiga na kitu kizito.
 
Naona VP kapooza sana
Ila Mwinyi analeta ma deal mengi
Wale wafanyabishara wa Kariakoo wanajenga hoja kwa sauti, pumzi na msisitizo kiasi kwamba inaeleweka ila kuna viongozi wakubwa nchi hii hata sauti zao hazijulikani. Ninajua ni Watanzania wengi sana hawawezi tambua sauti ya VP wakimsikia anaongea bila kujitambulisha au kumuona
 
VP ni spare tyre na kama hakuna hitilafu kwny matairi yeye hana kazi

hata Samia akiwa Makamu alikuwa hana kazi
Basi hakuna umuhimu wa VP ila kufuja hela za walala hoi tu
Yaani ni kama yule wa zamani ambae utamuona wakati wa ufunguzi tu anapopewa Mkasi basi
 
Wale wafanyabishara wa Kariakoo wanajenga hoja kwa sauti, pumzi na msisitizo kiasi kwamba inaeleweka ila kuna viongozi wakubwa nchi hii hata sauti zao hazijulikani. Ninajua ni Watanzania wengi sana hawawezi tambua sauti ya VP wakimsikia anaongea bila kujitambulisha au kumuona
Hicho cheo kingeondolewa tu
VP hasikiki kabisa na asilimia kubwa nchini hawamjui mpaka ajitambulishe FACT
 
Basi hakuna umuhimu wa VP ila kufuja hela za walala hoi tu
Yaani ni kama yule wa zamani ambae utamuona wakati wa ufunguzi tu anapopewa Mkasi basi
kwa hiyo Wewe kama hujawahi kuharibikiwa na Tyre kwa muda mrefu basi ndio tutasema huna haja ya kununua Jeki ya bei mbaya?

Makamu wa Rais ni kama Bima …unaweza ukalipa miaka mingi usione faida yake lakini kuna siku utahitaji hiyo spare

rejea ya March, 2021
 
Tumeshazoea Rais wetu akibanwa anampeleka Mwinyi kumuwakilisha katika shughuli na vikao vya nje ya nchi,

Mfano leo Dk. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar kuelekea nchini Qatar kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kimataifa la tatu la uchumi linalofanyika Jijini Doha. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya Washiriki ikiwa ni pamoja na Viongozi wa kampuni kubwa duniani na Viongozi wa juu wa Serikali.

Phillip Mpango hayupo, kawekwa kuwa pambo au?
Watu wajinga Huwa hamkosekani
Hata mwezi haujaisha VP amesafiri safari 3 Nje ya Nchi tofauti na Rais wa Zanzibar au PM ambao husafiri mara chache sana kumuwakilisha Rais.
 
Hapana si sawa. Maana katiba rais wa Zanzibar ni sawa na mkuu wa mkoa wa Katavi.
 
Tumeshazoea Rais wetu akibanwa anampeleka Mwinyi kumuwakilisha katika shughuli na vikao vya nje ya nchi,

Mfano leo Dk. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar kuelekea nchini Qatar kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kimataifa la tatu la uchumi linalofanyika Jijini Doha. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya Washiriki ikiwa ni pamoja na Viongozi wa kampuni kubwa duniani na Viongozi wa juu wa Serikali.

Phillip Mpango hayupo, kawekwa kuwa pambo au?
mdogo wangu ngoja nikutume ili uzoee haya majukumu ikifika ule mwaka nikuachie uje huku upande wa pili mimi nishachoka nataka nikalee wajukuu.
 
Back
Top Bottom