Rais wasaidie wananchi wako Viziwaziwa mkoa wa Pwani

Rais wasaidie wananchi wako Viziwaziwa mkoa wa Pwani

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,057
Reaction score
7,611
Tunajua kuna Nguvu kubwa sawa na ile kanuni ya Newton 3rd law of motion maana kila hili likiwekwa hapa wahusika wanajitahidi nao kulizima, moderator mnapaswa kuwa sauti ya wasio na sauti kwa kweli maana hili jukwaa ni huru.

Hoja ni hii, wakazi ndani ya mtaa wa Viziwa ziwa (VIMISA) Kibaha mjini wanahujumiwa sana. Kuna hari ya sintofahamu sana na viongozi kuanzia ngazi ya mtaa wa Viziwaziwa hadi H/mashauri wanashiriki hujuma hii kwa wananchi.

Kupitia mamlaka zako Raisi wananchi wanaomba uwasaidie kama ni kupitia kwa waziri husika, mkuu wa wilaya ama hata waziri mkuu ilimradi waache kunyanyaswa na kuonewa hivi, wanataka kuvunjiwa nyumba zao na mwekezaji ambaye anadai eneo lina watu 400 tu na eti wamejenga mabanda na si nyumba wakati ukweli ni kwamba eneo lina wananchi zaidi ya 700 na wamejenga nyumba zao za thamani na si vibanda kama inavyodaiwa. Imekuwa kila siku ni kutishiwa na hata kunyimwa huduma za kijamii kama maji, barabara na umeme wakati katika shughuli za mtaa wanashiriki wakiwa mstari wa mbele.

Najua na hii itafutwa lakini mwenye kuusoma ujumbe huu basi awasaidie wananchi hawa hima kwa namna anavyoweza kujaaliwa, mateso kwa hawa watu si ya kibinadamu asilani abadani
 
Back
Top Bottom