Rais wetu, fahari yetu, kazi iendelee

Rais wetu, fahari yetu, kazi iendelee

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan. Ni mwenye kusikia kama Jina lake linavyosadifu, amesikia kero za wananchi wake na amezitatua kwa kiwango kikubwa na bado anaendelelea amehakikisha kero za Elimu, afya na Lishe, maji, miundo mbinu, biashara na viwanda, Utunzajiwa wa mazingira na kuhamasisha matumizi ya nishati safi, nishati na madini, usafirishaji, kilimo, mifugo na uvuvi anaendelea kutatua kwa kuongeza bajeti na wataalamu katika maeneo husika ili kuweka mazingira bora kwa wananchi wa Tanzania.

Pamoja na jitihada zote anazoendelea kuzifanya majanga ya asili nayo hayakubakia nyuma. Mambo ambayo yapo nje ya uwezo wa mwanadamu kuweza kuzuia kwani muumba wa mbingu na ardhi akitaka jambo kuwa basi huwa. Mfano wa majanga hayo ya hivi karibuni Mafuriko ya Lindi, Rufiji, Arusha, na maeneo mengine na maporoko ya mlima kule Mbeya. Mungu awape faraja wote walipoatwa na changamoto hii. Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dr Samia na wadau mbalimbali wamepeleka misaada mbalimbali kuwasaidia waathirika wa majanga haya. Tanzania Hatuna budi kuliombea taifa letu, mungu atuepushe na kila aina ya maafa, njaa, magonjwa na vita. Ajaalie amani na utulivu, amlinde Rais wetui Dr Samia suluhu hassan na kila aina ya shari pamoja na wasaidizi wake. Amiin🙏

Wapo viumbe wachache wasiomtakia kheri Raisi wetu na wasiokuwa na adabu na maadili mema wanatumia muda wao kumtukana katika mitandao ya kijamii. Rais Dr Samia ni mama yetu, kipenzi cha watanzani. Hivyo hatuna budi kutunza utu wa kiongozi wetu mwenye hekima na busara, mwenye hofu ya mungu, anaipambania haki ya kila mtanzania. Ni jukumu letu sote kumlinda na kumheshimu kama katiba yetu ilivyotuelekeza. Sisi watanzania tunawajibu wa kumzungumiza vyema kiongozi wetu, bila kumbeza, kumdhihaki, kumdhalilisha na kumdhania yasiyokuwa mazuri ili kumkatiza tamaa asisonge mbele katika kulitumikia taifa hili. Tutasimama na Raisi wetu Dr Samia Suluhu Hassani tutamlinda na tutazidi Kumuombea dua mungu amlinde. Mungu Ibariki Tanzania. Dr Samia Mitano tena

📍15 Aprili 2024
Na
Mwajabu Rajabu Mbwambo
Mwenyekiti Uwt Mkoa Dar es salaam
#Dr Samia Mitano Tena 2025

WhatsApp Image 2024-04-15 at 13.30.30.jpeg
 
Back
Top Bottom