Rais wetu Hersi kwanini unaruhusu wanasiasa waingie kupenyeza agenda zao za kisiasa Yanga?

Jbst

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2020
Posts
1,971
Reaction score
4,085
Nimefikiria sana huu upumbavu anaoukubali rais wetu wa Yanga !! Hivi Kweli yanga inahitaji hamasa za kisiasa kushinda mechi? Kiukweli ni hapana.

Sijawahi kuona au kusikia popote kutoka kwa wenzetu waliofanikiwa ktk soka kukubali team zao kutumiwa kisiasa na watawala. Ni mambo ya hovyo sana.

Hili swala sio ushabiki wa kisiasa kwamba naichukia CCM, hapana. Ila huu upumbavu tunapaswa kuukataa na sio kwa Yanga tu hata simba inapaswa kukataa huu upuuzi.

Hata zile pesa sijui za kila goli hazina maana yoyote na haziwezi kuhamasisha team kushinda mechi,

Nimeshangaa sana viongozi wa serikali kusafiri na team tena wakiwakalisha wachezaji kuwambia porojo zao za kisiasa ili kushinda mechi!

Huyu hersi ni Muoga tu alipaswa kuwakataa wanasiasa wote. Serikali kama kutoa hamasa walipaswa tu kutoa ndege basi au kutoa tu ahadi mkishinda mtapewa kiasi fulani, tena walipaswa kutoa hizo ahadi kwa rais hersi sio kwenda kuonana wachezaji kabla ya mechi.

Ukimsikiliza yule waziri ni porojo tupu na mweupe kabisa kuhusu mpira wa miguu sana sana kulikua na kampeni za kisiasa tu,

Kulikua na haja gani watu kuvalishwa nguo za mama samia?

Hii nchi imelaaniwa
 
Mimi si mwana Y.
Ila mambo mengine ni magumu sana .
 
Hata wavalishwe chupi kichwani hatokuwa tena kamwe iko hivo imeisha hio.
 
Hata sijasoma mkuu ila nipo na wewe kwa ulichosema we ndio shabiki sasa
 
utaumia sana wanasiasa ndio wenye timu, hujui tu!
 
Unaonesha upo mbali sana na dunia ya michezo.

Kitafute kisa cha Boris Johnson, waziri mkuu aliyepita wa Uingereza alifanya nini alipokuwa mayor wa London.
 
Nothing can be done , hata iwe Simba au team yoyote . Football washing ni duniani kote . You can’t separate football from politics .
 
Herisi pale kawekwa tu hivyo hana usemi

 
Mtoa mada unazifahamu kweli timu za Yanga na simba? Hata ungekuwa wewe ndiye rais wa Yanga, ungewaruhusu tu hao wanasiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…