BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amelikosoa bunge la Umoja wa Ulaya baada ya kuitaka serikali yake kusitisha mradi wa kimkakati wa bomba la mafuta na nchi jirani ya Tanzania.
Wiki mbili zilizopita wabunge wa Umoja wa Ulaya walipitisha azimio la onyo la ukiukwaji wa haki za binadamu na hatari ya kijamii na kimazingira inayoletwa na mradi huo.
"Baadhi ya wabunge hawa wa EU hawawezi kuvumilia na wana makosa kiasi kwamba wanafikiri wanajua kila kitu lakini wanapaswa kutulia," Bw Museveni alisema katika mkutano wa kila mwaka wa kilele wa kimataifa wa mafuta na gesi wa Uganda
Aliongeza: "Huu ndio uwanja wa vita usio sahihi kwao. Natumai washirika wetu wataungana nasi kwa uthabiti na kuwashauri. Kwetu sisi, tunaendelea na programu yetu."
Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema baadhi ya watu 100,000 wako katika hatari ya kuhamishwa makazi yao na wamewataka wakandarasi, Kampuni ya Total Energies ya Ufaransa na Shirika la Mafuta la China National Offshore Oil Corporation, kusitisha mradi wa $10bn (Tsh. Bilioni 23) hadi wapate njia mbadala.
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki utaenea kilomita 1,443 (maili 896) kutoka Ziwa Albert magharibi mwa Uganda hadi bandari ya Tanga ya Tanzania kwenye Bahari ya Hindi.