Rais Zelensky aomba tena kukutana na Rais Putin ili wamalize vita

Rais Zelensky aomba tena kukutana na Rais Putin ili wamalize vita

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ametoa tena wito wa kufanya mkutano na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika juhudi za kumaliza vita nchini mwake.

Zelensky ambaye alishawahi kuomba kukutana na kiongozi huyo amesema hakuwa na hofu ya kukutana na Putin iwapo hilo lingesababisha makubaliano ya amani kati ya mataifa hayo mawili.

Alituma maombi hayo jana Jumamosi Aprili 23, 2022 na kuongeza kuwa tangu mwanzo amekuwa akisisitiza mazungumzo na Rais Putin lakini amerudia onyo lake kuwa watavunja mazungumzo ikiwa Urusi itawaua wanajeshi wa Ukraine waliosalia katika bandari iliyozingirwa ya Bahari Nyeusi ya Mariupol.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken anatarajia kutua Ukraine, leo Jumapili, Aprili 24, 2022 siku ambayo uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine unaingia mwezi wa tatu.

Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amekataa kuzungumzia ziara hiyo ya kwanza rasmi ya maafisa wa serikali.

Rais Zelenskiy ameishutumu mipango ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kutembelea Moscow siku ya Jumanne, kabla ya Kyiv, akisema hakuna haki wala mantiki katika utaratibu huo.

Source: Ndtv


========================

Ukraine President Zelensky Calls For Meeting With Putin 'To End The War'

Kyiv: Ukrainian President Volodymyr Zelensky on Saturday called again for a meeting with Russian leader Vladimir Putin in an effort to "put an end to the war".

"I think that whoever started this war will be able to end it," he told a news conference at a metro station in the heart of the Ukrainian capital.

He was "not afraid to meet" Putin if it would lead to a peace deal between Russia and Ukraine, he added.

"From the beginning, I have insisted on talks with the Russian president," said Zelensky.

"It's not that I want (to meet him), it's that I have to meet him so as to settle this conflict by diplomatic means. We have confidence in our partners, but we have no confidence in Russia," he added.

US Secretary of State Antony Blinken will visit Kyiv Sunday, the day the Russian invasion of Ukraine enters its third month, President Volodymyr Zelensky said.

US Defense Secretary Lloyd Austin would also visit, he told reporters. It will be the first official visit by US government officials since the February 24 invasion.

A US State Department official declined to comment.
 
RFA walikuwa na msemo wao "MWENYE NGUVU MUITE POWER"
Ni ngumu sana kupambana na Russia.
 
Huyo zelensky fala tu, anaomba kuongea na Putin wa nini kati warussia wanakula kichapo Ukraine, fala sana huyo jamaa aache warussia wale kichapo mpaka wakome.🤣🤣🤣
 
kwahiyo Putin atakwenda huko kyiv kukutana na bwana Comedian
 
Back
Top Bottom