Rais Zelensky aomba watu duniani waandamane kuipinga Urusi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameomba dunia kuandamana kupinga operasheni ya Urusi nchini Ukraine. Operesheni ya Urusi nchini Ukraine imesababisha mapigano na vifo vya watu wengi tangu kuanza kwake Februari 24

Rais Zelensky amesema kuisapoti Ukraine ni kusapoti uhuru na Maisha. Ametaka watu waingie mitaani an viwanjani kufanya sauti zao zisikike kuhusu kupinga hatua za Urusi

Mgogoro wa Urusi na Ukraine umesababisha matatizo mengi duniani ikiwemo kupanda kwa bei za mafuta na chakula kwa nchi zinazoendelea
===
Zelensky Urges Global Protests Against Russia

The Ukrainian President has urged citizens around the world go out and protest against Russia's operation in Ukraine.

"Come with Ukrainian symbols to support Ukraine, to support freedom, to support life," Zelensky said in a video address in English. "Come to your squares, to your streets, make yourselves visible and heard."

RT News
Angekataa kujiunga na Nato kulikuwa na shida gani.ona wananchi wanavyoteseka.ujinga wake mwenyewe.
 
Kwani Ukraine iliposhiriki kuivamia Iraq , Nani aliandamana hapa duniani?

Israeli wanapoivamia palestina, wapi raia wa Ukraine waliandamana?
IMG_20220302_021455.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku kwetu tutachezeshwa virungu mpaka polisi tuwaone wanafanana na Putin..[emoji23]

By the way tunaanzia wapi maandamano kikubwa mbio ninazo bila kusahau na kidumu cha maji..[emoji28]
Tuwaachie Chadema. Wao ndio hawana kazi za kufanya. Kila siku wanalilia kuandamana. Fursa hiyo. Waitumie vizuri

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Ana utani!
Huku kwetu polisi wamemchakaza mungu Zumaridi, eti tuandamane!
Apambane na hali yake! Awahimize wananchi wake!

Wapambe wake, wanakutana huko 7 stars hotels, Kula BATA, Kwa kisingizio cha vikao kumjadili yeye na Vita iliyo kwake! Watampa bunduki na risasi Ila hawapeleki wanajeshi wao!

Idiot of a comedian!
 
kweli huyo rais ni mtu wa vichekesho na raia wa ukrein nao hawakuwa na utimamu wa akili kumchagua huyo comedian
sasa acha wakione cha moto na bora akamatwe na majeshi ya urusi halafu ndo atalijua jiji
 
Kwa nini Russia hataki Ukraine ijiunge NATO, tatizo kwa Russia ni nini ?

Na Russia anatoa hoja gani ya kusema ana haki ya kutaka jirani asiingie NATO?
 
Kwa nini Russia hataki Ukraine ijiunge NATO, tatizo kwa Russia ni nini ?

Russia anatoa hoja gani ya kusema ana haki ya kitaka jirani asiingie NATO?
Ni makubaliano yao ya mwanzo kipindi warsaw pact wanaivunja........shida mmoja anakiuka makubaliano ndo hapo shida inapokuja kwa mrusi
 
Kama ile ya US alokua nayo wakat wa CUBAN CRISIS
 
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameomba dunia kuandamana kupinga operasheni ya Urusi nchini Ukraine. Operesheni ya Urusi nchini Ukraine imesababisha mapigano na vifo vya watu wengi tangu kuanza kwake Februari 24

Rais Zelensky amesema kuisapoti Ukraine ni kusapoti uhuru na Maisha. Ametaka watu waingie mitaani an viwanjani kufanya sauti zao zisikike kuhusu kupinga hatua za Urusi

Mgogoro wa Urusi na Ukraine umesababisha matatizo mengi duniani ikiwemo kupanda kwa bei za mafuta na chakula kwa nchi zinazoendelea
===
Zelensky Urges Global Protests Against Russia

The Ukrainian President has urged citizens around the world go out and protest against Russia's operation in Ukraine.

"Come with Ukrainian symbols to support Ukraine, to support freedom, to support life," Zelensky said in a video address in English. "Come to your squares, to your streets, make yourselves visible and heard."

RT News
Huku kwetu maandamano ni mwiko., lakini nyoyo zetu zipo upande wa Ukraine, tunaelewa mulilala na asubuhi kuamkia mabomu kila upande, hii haikubaliki na ni jambo la kulaaniwa na kila mtu, sauti zetu tunapaza sana kupitia mitandao na tuna matumaini makubwa Ukraine watashinda hii vita na mwanga tayari ushaonekana juzi warusi wamefurushwa na kurudi nyuma walikotoka 100 kilometers, jana meli 3 za urusi zimeripuliw Kiev, Majenerali 5 wameenda na maji, siku zote tupo pamoja na nanyi, Zelensky ndio rais wa pekee kwa sasa anaestahili kuvanishwa nishani ya ujasiri kwa kuipigania nchi yake bila ya unafiki, tunakupenda sana 💪💪💪💪💪
 
Ni makubaliano yao ya mwanzo kipindi warsaw pact wanaivunja........shida mmoja anakiuka makubaliano ndo hapo shida inapokuja kwa mrusi
anhaaa

na hayo huwezi kuyasikia BBC, Deutch Welle, AP, AFP, VOA… CNN, SKY NEWS, FOX NEWS…

Yani wote wanaongea sauti moja ya Westerners…
 
Huku kwetu maandamano ni mwiko., lakini nyoyo zetu zipo upande wa Ukraine, tunaelewa mulilala na asubuhi kuamkia mabomu kila upande, hii haikubaliki na ni jambo la kulaaniwa na kila mtu, sauti zetu tunapaza sana kupitia mitandao na tuna matumaini makubwa Ukraine watashinda hii vita na mwanga tayari ushaonekana juzi warusi wamefurushwa na kurudi nyuma walikotoka 100 kilometers, jana meli 3 za urusi zimeripuliw Kiev, Majenerali 5 wameenda na maji, siku zote tupo pamoja na nanyi, Zelensky ndio rais wa pekee kwa sasa anaestahili kuvanishwa nishani ya ujasiri kwa kuipigania nchi yake bila ya unafiki, tunakupenda sana 💪💪💪💪💪

Sioni ajabu hata vita vya iraq, libya, Syria, Afghanistan na palestina ulishabikia wamagharibi!!! Au si hivyo!
 
Ni jamaa mmoja muhunu muhuni tu aliyeingizwa ikulu ya Ukraine na Mabeberu, hivyo don't be surprised kuona anayoyafanya maana anatimiza matakwa ya waliomuweka madarakani.
Sijui Anajikuta nani.Yaani ananikera. Aanze yeye kuandamana.
 
Back
Top Bottom