Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umetumwa itapendezaRaila amekuzwa kisiasa kwa posts kama hizi, yaani ukifuatilia maisha ya Raila, kawaida huwa hana chochote cha maana hata ukimskliza kwenye mahojiano au hotuba au kusoma jarida zake, sijamskia hata siku moja akionekana tofauti, na hata alipokua waziri mkuu, ofisi yake ilikumbwa na ufisadi na ukabila balaa.
Lakini ukweli ni kwamba Jubilee na serikali zote za hapo awali ndio zimemjenga kwa kuchochea mashambulizi dhidi yake, kila uchao unawaskia wakiongea kumhusu, mara Raila hiki, mara Raila kile, yaani hata rais Uhuru na Ruto hawamalizi siku mbili bila kuongea kumhusu, na hili Raila ameshalijua, ndio maana huwa anaibuka na kila aina ya vituko ili waendelee kumtaja taja maana huo ndio mtaji wake wa kisiasa.