Raisi awaidhinisha wahindi kama kabila la 44 nchini Kenya

Raisi awaidhinisha wahindi kama kabila la 44 nchini Kenya

Dah! Kiswahili chako huwa kibovu sana jamaa, kama Nyerere aliwaunganisha kwa kutumia Kiswahili, basi wewe alikusahau. Hivi wewe huwa unawasiliana kivipi, maana hujui Kingereza, halafu wengi wenu hamjui kuongea lugha zenu za asili, ilhali Kiswahili chenyewe unaandika majanga hadi unatia kichefuchefu.
Haha wewe unajua kingereza umeandika kingereza ndo nastajabu why hata Mimi nimeweza kusoma hali sijui kingereza

2 Timotheo:4.2
lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
 
Bora huyo Rais wa Kenya kaunganusha Wakenya na Kabila la wahindi. Huyu wa kwetu Mzee wa PhD feki anazidi kutugawa Watanzania kwa ukanda, ukabila na siasa!!


Huyu makufuli anakolipeleka Taifa ni Mungu tu ndiye anajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe hata wewe hujui!? Sasa kwa nini unalaumu

2 Timotheo:4.2
lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
 
Kwanza inafaa ikuingie kwamba nchi zetu hizi hazikua na watu tangia mwanzo, mababu zetu walihamia tu, labda huwa hampewi hiyo elimu shuleni, ni kwamba hayo makabila ya Tanzania yalihamia kutoka kwa mataifa mengine, Wanyamwezi waliingia Tanzania kwenye karne ya 17, huo ni mfano mmoja tu na kila kabila lina historia yake.

Hivyo sisi tulichokifanya kwa Wamakonde na hawa Wahindi ni kuidhinisha uwepo wa jamii zao na kuzitambua kikatiba kama jamii za Kenya. Wao walikuja tu kama jinsi jamii zingine zilivyokuja. Kwa mfano jamii yangu ya Wakikuyu walitokea kule Kongo, wakapitia hapo Tanzania na kuishi Kilimanjaro kwa zaidi ya miaka 1,000 ndio hatimaye wakahamia huku Kenya. Hivyo itakua unafiki kutotambua jamii zingine ambazo zilihamia huku kihivyo kabla Kenya haijawa taifa huru.

Nyie hapo mnajiita Watanzania leo, lakini hiyo ni baada ya mzungu kuja na kuchora chora mipaka baina ya Waafrika na kuanzia hapo akawaambia mjiite Watanzania au mwanzo Watanganyika, na sisi akatuambia tujiite Wakenya. Huko kwenu kuna jamii zaidi ya 120 zinazotambuliwa na katiba yenu, hivyo wacha kubwatuka maana hamna utofauti wowote na Waafrika wengine.
Tatizo ni kwamba nyie mumetelekeza tamaduni na asili zenu kiasi cha kuwa kama watumwa wasiojua historia au asili yao. Utakuata asilimia kubwa ya Watanzania hawajui hata kuamkuana kilugha, utumwa kabisa huo.


You are right.The first time I went Nairobi I was impressed to see atlist every Kenyan is fluent in 3 languages.Swahili,English and his/her mother tongue.
 
424c1ebf9684b7674b989edcd20a0fee.jpg
 
Nasi Rais Magufuli awaidhinisha Wahutu na Watusi kama Kabila la 123 Tanzania.

sent by Samson Cyper
 
Si kweli.

Nyerere hakukuta watu ambao hawajaungana,

Kiswahili alikikuta kinaongewa tayari hata kwao.

Msitake kuleta historia ambayo haikuwepo.
Alichokifanya Nyerere Sio kuunganisha kwa kiswahili yeye alichofanya aliua tawala zote za kikabila kama watemi na mangi then kawachangannya Watu mtoto wa mbeya anaenda kusoma moshi wa mwanza anasoma arusha wa moshi anaenda Dar nk. Na lugha hapo ni kiswahili so Watu wenyewe kwa kuchanganywa huko wakaoleana na kuungana kuwa kitu kimoja.
 
Back
Top Bottom