Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 887
Raisi Samia kafanya ziara nchini Korea ya kusini mapema leo, ntaingusia Korea kusini kidogo leo.
Nchi ya Korea kusini ilianzishwa mwaka 918, wakati wa mgawanyiko wa maeneo ya koo tatu zilizoitwa "Three Kingdoms" koo hizo zilikuwa ni ukoo wa Goryeo, ukoo wa Silla na ukoo wa Baekje.
Koo hizi zilizoitwa "Three kingdom", ziliunda utawala wao eneo ambalo leo ndio huitwa "Peninsula ya Korea" koo ya Silla ilianzisha wazo la kuunda dola moja, kwa kiasi ikafanikiwa ila baadae wazo hilo likianguka kutokana na wasaliti kadhaa, hapa kulipita mengi ntaeleza wakati mwingine.
Tuendelee na Korea kusini...
Jina Korea linatokana na Ukoo wa Goryeo kwasababu wao ndio walio fanikiwa kuanzishwa "muungano wa kweli wa kitaifa" wa taifa la Korea ya Leo.
Wanahistoria wanaeleza kuwa Jina "Korea" linatokana na jina la Goryeo, ambalo pia limetafsiriwa kama Koryŏ, ambalo lilitumiwa kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa karne ya 5 na ukoo wa Goguryeo.
Ukoo wa Goryeo ulikuwa dola iliyoitwa baadaye Goguryeo na baade Goguryeo, ndio ilianzisha nchi ya Korea yote yani kaskazini na kusini chini ya mfalme wa kwanza aliyeitwa Taejo of Joseon.
Turudi kwenye ziara ya Raisi Samia...
Raisi wetu Samia leo alipo wasili Korea kusini ameshukia uwanja wa ndege wa jeshi wa Sejong, uwanja huu umepewa jina hilo "Sejong" kurejea heshima ya mfalme wa nne wa Korea aliyeitwa Sejong the great.
Huyu Sejong the great ndie anaye chukuliwa kuwa mmoja wa watawala wakuu katika historia ya Korea na anakumbukwa kuwa mwanzilishi wa lahaja ya "Hangul" ambayo ndio iliyo zaa alfabeti ya asili ya lugha ya Kikorea.
Sasa Basi...
Mji mkuu mpya wa Korea kusini umepewa jina hilo la Sejong city, mji huu ulianziswa mwaka 2007, kama mji mkuu mpya wa Korea Kusini kutoka mkoa wa Chungcheong Kusini na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Chungcheong Kaskazini ili kupunguza msongamano katika jiji kuu la sasa la Korea Kusini na jiji kubwa la Seoul.
Tangu 2012, serikali ya Korea Kusini imehamisha wizara na mashirika mengi ya serekali hadi Sejong, lakini shughuli nyinginezo za serikali bado zimebakia Seoul hasa Bunge la Kitaifa na ikulu ya serikali iitwayo Blue House yamesalia Seoul.
Ziara ya Mama Samia imeanza katika jiji hili la Sejong, hapa ndio ataanza ziara yake.
Ndimi Comred Mbwana Allyamtu-CMCA
Friday -31/05/2024
Marangu Kilimanjaro Tanzania.
Soma:
- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51