SI KWELI Raisi Wa Uganda Yoweri Museni Anakabiliwa Na Hali Mbaya Hospitalini

SI KWELI Raisi Wa Uganda Yoweri Museni Anakabiliwa Na Hali Mbaya Hospitalini

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwa Na Taarifa Zinasambaa Kwenye Mitandao ya Kijamii Ususani Facebook Zikionesha Raisi wa Uganda Kuwa Yupo Hospital Na Anakabiliwa Na Hali Mbaya .Je Taarifa Hizi Zina Usahihi Kiasi Gani

1760820275884.jpg
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na taarifa zinazoeleza kuwa hali ya Rais wa Uganda na mgombea wa kiti cha Urais kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanika January 2026, Yoweri Museveni ana hali mbaya kiafya.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kutoka Uganda ama kimataifa kilichochapisha taarifa kuhusu Museveni kuwa na hali mbaya kiafya.

Ufuatiliaji wa kimtandao umebaini kuwa hata mamlaka za Uganda pia hazijachapisha taarifa hiyo mathalani ukurasa wa Ikulu ya Uganda katika mtandao wa X, hakuna taarifa yoyote ya hivi karibuni kumuhusu kiongozi huyo.

Kupitia ukurasa wake wa X, Rais Museveni alichapisha taarifa Oktoba 18, 2025 akieleza kuwa amekutana na wazee na viongozi kwa siku hiyo kutoka maeneo ya Moyo na Obongi na kujadiliana nao masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kutokomeza umasikini. Museveni aliandika;

"Today, I met elders and leaders from Moyo and Obongi at Arua State Lodge. I commend their commitment to fighting poverty through enterprise and focus on perennial crops like coffee, cocoa, avocado, and dairy. We’ll support them with seedlings under zonal production and the PDM. We also discussed cattle rustling and compensation for livestock raided by groups from South Sudan, government will follow up through OPM and the Attorney General."

Katika taarifa hiyo Museveni aliambatanisha pia na video inayomuonesha akizungumza na watu hao akiwa na afya njema.
Back
Top Bottom