Rally Bwalya ampishe Sharaf Eldin Ali AbdulRahman Shiboub

Rally Bwalya ampishe Sharaf Eldin Ali AbdulRahman Shiboub

Bwalya akicheza namba kumi bado anakuwa mzito Hana pass za maana ana slow down mashambuliz pia akicheza namba nane deep Line midfielder kuna mda anapafomu kuna mda anakuwa slowly na shallow Sana Yan haelewek
 
Kwa kifupi tu ukiachana na ujio wa Shiboub a.k.a Zenadine Zidane Zaizou,huyu Raly Bwalya likipatikana soko auzwe au atolewe kwa nkopo uyu ntu.
Aje awaulize wenzie kina lwanga alipigwa kanzu na maestro feisal mpka akavunjika mzee wa watu.
 
Mfumo wa kocha PABLO naiona kuwa ni soka la haraka haraka...
Ndo maana utaona wachezaji wenye kasi waking'ara kwa sasa .. Mfano ni Dilunga, KIBU , KANOUTE , Sakho. Kagere... ....Ajbu alifeli mfumo. Sijui kwa Mugalu ..ngoja tuone.
Bwalya aongeze kasi ya kukimbia , na pasi za mbele..
 
Bwalya ni mchezaji mzuri na anauwezo mkubwa wa kuuchezea mpira. Lakini iwapo mimi ningekuwa kocha ili nipate kitu bora kutoka kwake ningemtumia kama winga wa kulia au wa kushoto tu na hapo nitawaambia mabeki wangu wa pembeni wasipande hovyo kwa sababu Bwalya sio mzuri kwenye kurudi kukaba.

Japo Bwalya mwenyewe na hata makocha wake wanapenda sana kumtumia kama namba 8 na 10 lakini anakuwa mzigo sana kwa timu kwa sababu:-
1. Hakabi na hapendi kabisa kugongana kugombania mpira. Kwenye timu zinatotumia nguvu ndio hutamuona kabisa.
2. Anapenda sana kushuka sana chini kwenda kucheza mipira ambayo na 6 na mabeki wakati wanatakiwa waicheze wao ili kuwavuta wapinzani halafu ndio asogezewe yeye. Matokeo timu ikianza kupanda kushambulia unakuta yeye yupo chini kabisa kwa hiyo anawapa kazi sana mawinga na washambuliaji wa kati.
3. Yupo taratibu sana hata wakati timu inapokuwa inaenda kushambulia kwa kasi. Kwa mfano kwenye mechi ya jana dhidi ya Azama timu ya Simba walikuwa na kasi sana kule mbele lakini mpira ukifika kwa Bwalya alikuwa ana "slow" timu. Iwapo benchi la ufundi lingegundua mapema lilipaswa limuingize Dilunga ili aendane na kasi ya Sakho na Kibu ingewasaidia wangepata ushindi mapema sana.
4. Wakati Bwalya anaanza kucheza Simba alikuwa anaweza sana kupiga pasi za mbali tena kwa usahihi mkubwa lakini sasa hivi sijui kalogwa yaani akipata mpira utakuta anapiga vipasi vifupi vifupi tu hapo hapo tena mara nyingi za kurudi nyuma wakati yeye ndio anatakiwa aendeshe timu iende mbele.
5. Ana tatizo la pumzi. Akianza mechi ikifika dakika ya 60 hoi kabisa upepo umekata.

Lakini pamoja na yote hayo bado Bwalya anabaki kuwa ni mmoja wa wachezaji wachache waliopo Simba inaweza kuwatumia iwapo itakutana na timu zinazopaki basi. Ana uwezo mkubwa sana "ku unlock" difensi ya timu pinzani iliyopaki basi. Na ni vizuri kwake Bwalya mwenyewe akarudi akatazama jinsi alivyokuwa anacheza mechi za mwanzoni wakati anaingia Simba halafu akalinganisha na jinsi anavyocheza sasa nina hakika kabisa yeye mwenyewe ataona tofauti kubwa sana.
 
Hivi Kanoute ana speed!! The guy is very slow just like Mkude
Mfumo wa kocha PABLO naiona kuwa ni soka la haraka haraka...
Ndo maana utaona wachezaji wenye kasi waking'ara kwa sasa .. Mfano ni Dilunga, KIBU , KANOUTE , Sakho. Kagere... ....Ajbu alifeli mfumo. Sijui kwa Mugalu ..ngoja tuone.
Bwalya aongeze kasi ya kukimbia , na pasi za mbele..
 
IMG_3094.jpg
 
Bwalya na hasani dilunga ni wachezaji wazuri ila wakitokea benchi.
 
Mfumo wa kocha PABLO naiona kuwa ni soka la haraka haraka...
Ndo maana utaona wachezaji wenye kasi waking'ara kwa sasa .. Mfano ni Dilunga, KIBU , KANOUTE , Sakho. Kagere... ....Ajbu alifeli mfumo. Sijui kwa Mugalu ..ngoja tuone.
Bwalya aongeze kasi ya kukimbia , na pasi za mbele..
Hii style pale ulaya inaitwa gegen pressing mamaeee.....simba tamu nyie
 
Back
Top Bottom