OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Bongo tuna wachambuzi wengi na wengine maarufu sana. Wachambuzi wengi maarufu ni wa kawaida sana wanasimulia hadithi badala ya kuchambua. Wanaeleza matukio ambayo hata mimi mtu wa kawaida kwenye tasnia nayajua.
Lakini kuna mwamba Ramadhani Mbwaduke, huyu ni shujaa asiyeimbwa. Huyu sasa ndio mchambuzi raha sana kumsikiliza kwa sababu anakupa vitu usivyojua.
Hapa bado hajakupa takwimu. Huwa nafikiria kama akili yake ya kukariri takwimu angeitumia kwenye mambo mengine angefika wapi?
Binafsi hutazama kipindi cha Sport AM cha Binzubeir kwa ajili ya kumsikiliza Bwaduke tu.
Binzubeir kama unanisoma humu, kesho kwenye kipindi cha Sport AM mwambie Mbwaduke namkubali sana. Ni shujaa asiyeimbwa