Ramadhan Hamis Ntunzwe azidi kuanika Madudu ya TRA. Amwangukia Rais Samia

Ramadhan Hamis Ntunzwe azidi kuanika Madudu ya TRA. Amwangukia Rais Samia

TRA ni intarahamwe...Hao Commisioners na Manaibu wao wafumuliwe wote. Majambazi wahuni. Yaani Cartel kabisa
Njia nzuri ni kuonesha kiasi cha kodi na sio ukadiriaji hii itaondoa pia ishu za upigaji kutoka hao tra na gangs wenzao
 
Huyu mtu ameteswa sana. Na kwa kipindi kirefu amebugudhiwa kwa mura mrefu sana. Je ni ujumbe gani wanaituma kwa walipa kodi na wafanya biashara wengine? Viongozi wa kisiasa na kiserikali wapo ?

Maelekezo ya Rais, Naibu Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Fedha yanadhauliwa. Je, sisi wengine vipi?

=====

Mfanyabiashara Ramadhan Hamis Ntunzwe wa Dar es Salaam amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumsaidia kuiagiza Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kumlipa fidia baada ya TRA kumsababishia hasara ya zaidi ya Sh milioni 800.

Hatua hiyo imekuja baada ya kupita miaka miwili na ushee tangu Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli alipoingilia kati sakata hilo na kuagiza Mamlaka hiyo kumlipa fidia hiyo.

Licha ya kwamba Rais Magufuli alitoa agizo hilo tarehe 7 Juni 2019, pamoja na vikao mbalimbali vilivyofanyika kabla ya Rais Magufuli kufariki tarehe 17 Machi, 2021, hadi sasa hakuna fedha yoyote aliyolipwa.

Sakata la Ntunzwe linaanzia 2017 alipokuwa akisafirisha mzigo wake kutoka Zambia kupitia mpaka wa Tunduma. Baada ya kufika Mbezi, Dar es Salaam, alikamatwa na maofisa wa TRA waliomdai rushwa ya Sh milioni mbili lakini alikataa kuwapa fedha hizo.


Baadaye suala hilo lilichukua sura mpya baada ya maofisa hao wa TRA kumbambikia makosa ya kukwepa kodi na hatimaye kutaifisha mali zake, huku nyingine zikiharibiwa na kuporwa fedha taslimu kiasi cha Sh milioni 60.

Ntunzwe anadai kuwa hasara ya kutaifishwa na kuharibiwa mali zake katika jaribio la mali hizo kupigwa mnada na kuibiwa kwa fedha taslimu, vilimsababishia hasara inayofikia Sh milioni 821.

Aidha, akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Januari, 2022 jijini Dar es Salaam, Mfanyabiashara Ramadhan Hamis Ntunzwe baada ya agizo hilo la Rais Magufuli wakati huo, tarehe 26 Novemba, 2020 alipigiwa simu na ofisa kutoka wizara ya fedha na mipango kufahamishwa kuhusu taarifa ya kikao kati yake na Kaimu Katibu mkuu wa wizara hiyo.

Amesema kikao hicho cha kwanza kilichohusisha maofisa kutoka wizara ya fedha na TRA, kilifanyika tarehe 2 Disemba 2020, ambapo Katibu mkuu huyo alimueleza kuwa kutafanyika vikao vitatu pekee kisha atalipwa pesa yake.

Amesema katika maelezo ya katibu mkuu huyo, alimhoji iwapo ameishtaki TRA mahakamani au lah, lakini alijibu kuwa hajawahi kuishtaki TRA bali mamlaka hiyo pamoja na kampuni moja ya udalali ndio iliyomshtaki lakini katika kesi hiyo aliwashinda.

Mfanyabiashara huyo ameendelea kutiririka kuwa, baada ya kutoa majibu hayo kikaoni, mwanasheria wa TRA aliyehudhuria kikao hicho alishikilia msimamo kuwa mfanyabiashara huyo ndiye aliyewashtaki na wala si TRA iliyomshtaki.


Amesema kutokana na mabiashano hayo kikao hicho kiliahihirishwa hadi tarehe 15 Februari 2021 ambapo aliwasilisha hati ya hukumu ya kesi hiyo aliyokuwa ameshtakiwa na TRA kisha mwanasheria huyo wa mamlaka hiyo akakiri katika kikao cha kwanza alikuwa ameghafirika.

Amesema baada ya maelezo hayo kikao hicho kilifikia maamuzi ya kuahirisha kikao hicho cha pili ambacho kilifanyika jijini Dar es Salaam ambapo katibu mkuu huyo wa wizara ya fedha aliahidi katika kikao cha tatu ambacho kitafanyikas Dodoma ndipo maamuzi ya kulipwa pesa yake yatafikiwa.

Amesema kwa bahati mbaya, msiba wa kitaifa uliotokea tarehe 17 Machi ulisababisha kikao hicho cha tatu kutofanyika.

Amesema alisubiri hadi Juni mwaka jana ambapo aliandikia barua wizara ya fedha kukumbushia ahadi ya malipo yake katika kikao cha tatu lakini hakujibiwa.

Amesema hata alipoandika barua nyingine Agosti kwenda kwa waziri mkuu na Rais bado hakujibiwa.

“Kutokana na hali hiyo, namuomba Rais Samia kwa kuwa ni mtu wa Mungu asiyependa kuona wananchi wake wakidhulumiwa, namuomba sana anisaidie nilipiwe haki yangu. Hiio ni fidia ambayo nimepoteza fedha nyingi,” amesema.


Amesema licha ya madhila yote hayo, bado amekuwa akiandamwa na matapeli ambao wamekuwa wakimdanganya kuwa wametumwa na viongozi mbalimbali wa serikali jambo ambalo si kweli.

Pia, soma;

Sakata la RAMADHAN HAMIS NTUNZWE na TRA ni vijana chini 27

Mfanyabiashara Ramadhan Hamis Ntunzwe, adai TRA hawajatekeleza agizo la Rais. Je, Kamishna Mkuu TRA afukuzwe kazi na Yono ifilisiwe mali zake?


Yaani huyu mtu hajalipwa hadi leo?
 
Yaani unapambana kwa nguvu zote alafu serikali na watu wachache wanakukwamisha bila sababu za msingi.
Wakati hata wao wangepata faida vilevile kutokana na huyo jamaa.

Sidhani kama nakosea kusema Serikali ndio kikwazo cha maendeleo kwa wananchi wake na maendeleo ya nchi kiujumla.
 
Msikilize kwanza nikisema niandike yote aliyoongea kwenye huo mkutano wake huyo bwana basi kama gazeti limekuchosha; kuelezea A-Z ni kitabu.

Hivi unadhani raisi ana muda wa kusikiliza individual cases za kila mtu akishatolea maamuzi especially mtu kama Magufuli ambae kila akisimama anakutana na kesi jumlisha na majukumu yake mengine.

Jamaa ni kama anakumbushia tu serikali haki yake ajaipata bado.
Maneno meeeeeeeeeeeeeeeengi
 
Yaani unapambana kwa nguvu zote alafu serikali na watu wachache wanakukwamisha bila sababu za msingi.
Wakati hata wao wangepata faida vilevile kutokana na huyo jamaa.

Sidhani kama nakosea kusema Serikali ndio kikwazo cha maendeleo kwa wananchi wake na maendeleo ya nchi kiujumla.
Mijitu kama hao utakuta inanenepeana kwa fedha za dhulma tu

Ova
 
Inasikitisha na kuhuzunisha sana.
Kupitia Jf nilisoma sakata la mdai dhidi ya TRA. Ukimsikiliza kwa makini utagundua anachoeleza ni ukweli tupu, tena yawezekana wapo wafanyabiashara wengi wali/ wanaofanyiwa unyanyasaji wa aina hiyo lakini hawajapata nafasi ya kuueleza Umma.
Jambo la kusikitisha ni namna anavyozungushwa kupata Haki yake licha ya viongozi wa juu Serikalini kuagiza alipwe stahiki zake.
Inaumiza
 
Mmh hii nchi ngumu sana .. Nami nina ishu yangu na mamlaka ya mapato ina miaka nane sasa ya sarakasi, vitimbwi, ahadi hewa, kuzungushwa nknk.. ikifanikiwa kwisha nitakuja hapa na full mkanda
Hao wanajiita tra wengi wao wanaishi/kupata pesa zao kwa dhuluma tu

Ova
 
Inasikitisha na kuhuzunisha sana.
Kupitia Jf nilisoma sakata la mdai dhidi ya TRA. Ukimsikiliza kwa makini utagundua anachoeleza ni ukweli tupu, tena yawezekana wapo wafanyabiashara wengi wali/ wanaofanyiwa unyanyasaji wa aina hiyo lakini hawajapata nafasi ya kuueleza Umma.
Jambo la kusikitisha ni namna anavyozungushwa kupata Haki yake licha ya viongozi wa juu Serikalini kuagiza alipwe stahiki zake.
Inaumiza
Alafu kwenye kila mazungumzo yake habadilishi maelezo,jamaa ana kumbukumbu kali sana

Ova
 
Kama vipi nae aende TiaRa.A akafanye kama ya braza hamza(RIP)
 
Back
Top Bottom