Ramadhan Kayoko, Leo umetupa somo muhimu kiuamuzi

Ramadhan Kayoko, Leo umetupa somo muhimu kiuamuzi

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Tuisila Kisinda anapewa pasi na Fiston Mayele hatua chache toka katikati ya uwanja kuelekea lango la Mbeya City. Anakokota mpira kuelekea pembeni huku kila Mtu akiamini lengo lake ni kupiga krosi. Ghafla anakatisha kuingia kati na kuamua kushoot na mpira unampita kipa na kuingia wavuni.

Mshika kibendera aliyekuwa pembeni sambamba na mchezaji wa mwisho wa pili (Second last defender) wa Mbeya City anarudi katikati kuashiria goli ni halali turudi tuanze mpira. Awali Kayoko anaonekana kukubaliana naye kwa kuonyesha mkono wake wa kulia mpira upelekwe kati, lakini ghafla anabadili maamuzi na kunyoosha mkono juu kuashiria kuna mushikeri kwenye uhalali wa bao hilo, anamnyooshea mkono Mayele na kumwambia wewe uliingilia mchezo ukiwa offside.

Hili ni somo muhimu sana kwetu. Kumbe mwamuzi wa kati anaweza kumpinga mshika kibendera kuhusu offside na akaamua vinginevyo ikaonekana hakuna shida.

Waamuzi wengine wajifunze kwa Kayoko, si kila maamuzi ya offside yategemee mshika kibendera, kama unaona anazingua badili maamuzi maana mwisho wa siku utalaumiwa wewe mwamuzi wa kati.

Asante KAYOKO kwa somo zuri.
 
Alichokifanya refa ni jambo la kipuuzi na uzembe. Kama ulishaonyesha ishara ya mpira uwekwe kati na Line 1 hakua na shida na Goli lililofungwa naye amekwenda kati, wewe refa unatoa wapi ujasili wa kubadili maamuzi na kukataa goli bila kushauriana na Line 1.
 
Alichokifanya refa ni jambo la kipuuzi na uzembe. Kama ulishaonyesha ishara ya mpira uwekwe kati na Line 1 hakua na shida na Goli lililofungwa naye amekwenda kati, wewe refa unatoa wapi ujasili wa kubadili maamuzi na kukataa goli bila kushauriana na Line 1.
Inawezekana alikumbuka aliyofundishwa juzi. Si walikuwa na semina ya siku 5 wakifundwa jinsi ya kuona offside?
 
Kayoko ni refa Bora,
Haijusiani na ttzo la Jana, ila awe na maamuzi ya pamoja na line zngine yey peyake hawezi toa maamuzi sahihi
 
Huyu dogo mwanzoni niliamini ni mwamuzi bora kijana! Ila kupitia ile mechi aliyochezesha kati ya Yanga na simba, na hiyo ya jana; ni ushahudi tosha hana hizo sifa.

Na kosa lake kubwa nililo ligundua; ni kutozingatia sheria 17 za mpira wa miguu. Dogo anaonekana hafurahushwi kabisa na mafanikio/matokeo ya Yanga, ya ndani na nje ya uwanja.
 
Sasa refa wa kati unajuaje ni offside? Akubali tu kaouyanga au alkua na nia ya kuinyonga yanga ili watu flani wapate ahueni na kama Yanga asingeongeza goli angefunika tuta kuibeba Mbeya City
Hakuna mahali popote panapompa refa mamlaka ya kwenda kunyume na maamuzi ya marefa wasaidizi.Kama wamepatia safi na kama wamekosea unakuwa msala wao na refa hatalaumiwa.
 
Back
Top Bottom