Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Jamani tupo katka kukumbushan katk yale yaliyo mema na kukatazana katka yale yasiofaa pia usione aibu kuuliza chochote ambacho hukifaham wanaokijua watakufahamisha jaman hapa ktk swala pana mambo mengi sana ya kustaajabisha na ya kushangaza pia mtu ukiona swala yakushinda namanisha huiwez au hujui yanayotamkwa pindi mtu anapokuwa anaswali please jamn uliza au kam waon haya mfate mtu pm akufahamishe zaid Jamani kuhusu kutia udhu pia kwa baadhi ya waislam ni tatizo uliza sote tupo hap kwa ajil ya kujifunza ukion aibu kuuliz hap unawez kwenda pm ya yoyote na swala lako likawekwa mezan tukajadil MWENYEZI MUNGU NDO MUWEZA WA YOTE WABILLAH TAUFFIK ASALAM ALYKUM WARAHMA TULLAH WABARAKATUH
 
Nilisahau kuwa uzi unalenga watu wa dini moja nikajikuta naufungua na kuusoma.Mniwie radhi japo naamini kila mtu ana haki ya kupata elimu juu ya mwezi mtukufu,kwaresma au mifungo mingine.Na nadhani anayehitaji zaidi elimu yenu hiyo kuhusu uislam ni mtu asiyejua kitu.
 
Mkuu sala haiondoi funga

Hizo ni ibada mbili tofauti

Ila inashauriwa ukifunga uswali maana utapata thawabu nyingi sana

Ila ukifunga na usiswali funga yako inakubalika kama kawaida cha muhimu uwe umetia nia na umejizuia na yale yote yanayotengua funga.
Ndugu yangu katika imani, hapa umekosea, Swala ndio amali inayobeba amali zote baada ya kuamini kwa kutoa shahada, Muhimili mkuu wa matendo ni swala kama huswali, hukubaliwi sio tu swaumu hata hijja yako haikubaliwi.
 
Asalam alykum warahma tullah wabarakatuh

239ba22642d827d349ba52d25211c6ab.jpg
 
Nawatakia Ramadhan njema. Ila nina ombi moja.

Naomba yale mema mnayoyatenda kipindi cha Ramadhan yaendelee hivyo hivyo hata mwisho wa Ramadhan. Matendo mema yawe ni desturi na kawaida. Vinginevyo nadhani itakua ni sawa na kushinda njaa tu.
Ombi hili ni kwa ndugu zangu wakristo pia
 
Assalam aleykum warahmatullah wabarakatuh, Naomba kufahamishwa mambo yanayobatilisha funga,pili je kwa mfano mwanafunz kakosa ukamchapa /kumtoa ktk kipindi (kwa utovu wa nidhamu) huku ukiwa kwenye funga inabatilisha funga yako? Maana dunia imejawa na mitihani esp ktk hizi kazi za duniya
 
Yaliyo Muhimu Kwa Ujumla Wa Kutekeleza ´Ibaadah Ya Swawm (Kufunga)


1. Niyyah.
Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Amesema:

ﻭَﻣَﺎ ﺃُﻣِﺮُﻭﺍ ﺇِﻟَّﺎ ﻟِﻴَﻌْﺒُﺪُﻭﺍ ﺍﻟﻠَّﻪَ ﻣُﺨْﻠِﺼِﻴﻦَ ﻟَﻪُ ﺍﻟﺪِّﻳﻦَ ﺣُﻨَﻔَﺎﺀ ﻭَﻳُﻘِﻴﻤُﻮﺍ ﺍﻟﺼَّﻠَﺎﺓَ ﻭَﻳُﺆْﺗُﻮﺍ ﺍﻟﺰَّﻛَﺎﺓَ ﻭَﺫَﻟِﻚَ ﺩِﻳﻦُ ﺍﻟْﻘَﻴِّﻤَﺔِ


“Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Allaah kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Swalah, na watoe Zakaah. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.”
(Suuratul Bayyinah 98 : 05)


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:

’’Kila kitendo hulipwa (kutokana na) niyyah na kila mtu ni lili alilonuwiya.’’
Na niyyah mahala pake ni moyoni. Niyyah ya kufunga ni lazima iwe moyoni kila usiku kabla ya wakati wa Fajr kuingiya.
Hafsah (Radhiya Allaahu ´anha) amesema mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:

‘’Hana swawm asiyenuwia kufunga kabla ya fajr.’’

[Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jamiy´ as-Saghiyr, na.6238. Pia imerikodiwa na Abu Dawuud, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy].


2. Kujiepusha katika masiku ya kuamka na swawm na chochote chenye kubatilisha swawm yako (tangu wakati wa adhaana ya pili) na usiku mpaka kutakapopambauka (Jua kuchomoza).


Amesema Allaah (Subhanahu wa Ta’ala):

ﻭَﻛُﻠُﻮﺍْ ﻭَﺍﺷْﺮَﺑُﻮﺍْ ﺣَﺘَّﻰ ﻳَﺘَﺒَﻴَّﻦَ ﻟَﻜُﻢُ ﺍﻟْﺨَﻴْﻂُ ﺍﻷَﺑْﻴَﺾُ ﻣِﻦَ ﺍﻟْﺨَﻴْﻂِ ﺍﻷَﺳْﻮَﺩِ ﻣِﻦَ ﺍﻟْﻔَﺠْﺮِ ﺛُﻢَّ ﺃَﺗِﻤُّﻮﺍْ ﺍﻟﺼِّﻴَﺎﻡَ ﺇِﻟَﻰ ﺍﻟَّﻠﻴْﻞِ


“Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni swawm mpaka usiku.”
(Suuratul-Baqarah: 187).
 
Back
Top Bottom