Ramadhan Special Thread

Ewe mja wa Allah

Hakika kufunga sio kazi Sana,,,, kazi ipo katika kulinda swaumu yako au funga yako

Katika mfumo wa hadith Mtume rehma na amani ziwe juu yake anasema yule ambaye hataacha kusema uwongo na maneno ya kipuuzi basi hana haja ya kuacha Chakula chake na kinywaji chake.

Hapa ina maana mtu huyu hana funga kwahiyo ni bora siku hiyo angekula maana anashinda tu njaa bure

Kwahiyo tujichunge sana mienendo yetu katika kipindi hiki cha ramadhani ili funga ziwe zenye kukubaliwa.
 
Ramadhaan ni mwezi uliyochaguliwa na Muumba kwa ajili ya kuwatakasa waja wake waliyochagua kufuata maamrisho yake, ibada kuu ya mwezi huu ni kujizuia kula, kunywa na kukidhi matamanio ya nafsi kutoka panapoingia alfajiri ya kweli mpaka kuzama kwa jua. Ibada hii ina umuhimu wake kiimani, kiafya hata kiuchumi ikiwa itatekelezwa ipasavyo. Kitu kikubwa ni kila mwenye kufunga ajaribu kufuata kwa kadri awezavyo maamrisho na kujiepusha na makatazo ambayo yataweza kumfanya funga yake isiwe na tija iliyokusudiwa.
 
Nyakati Tatu Muhimu za Kupata Fadhila Kubwa

Ndg zangu katika imani nyakati hizi tatu ni muhimu sana katika miezi yote lkn wakati huu wa  Ramadhani ndio bora zaidi kwani malipo yake ni marudufu na fadhila zake ni nyingi mno.

Kwanza,,,baina ya alfajiri na jua kuchomoza

Huu ni wakati ambao Allah anasema tumdhukuru kwa wingi na kumsifu kwa wingi, kwahiyo nyakati kama hizi sio za kuzipuuza hata kidogo,,,, Mtume rehma na amani ziwe juu yake pamoja na masahaba wake walikuwa na kawaida mara baada ya kuswali alfajir basi hawaondoki misikitini hubakia wakifanya adhkar mbali mbali

Wakati wa pili

Ni kabla ya kuzama kwa jua (magharibi)

Huu nao ni wakati ambao Allah amesisitiza akumbukwe kwa wingi na kutukuzwa
Ni wakati mzuri mja wa Allah bado yupo kwenye swaumu na hivyo dua yake hupokelewa.

Mtume rehma na amani ziwe juu yake amesema Watu watatu dua zao hazirudi, mtu aliyefunga mpaka afuturu, kiongozi muadilifu na tatu mtu aliyedhulumiwa na kutaka msaada

Wakati wa Tatu


Wakati wa suhurw kabla ya alfajiri

Wakati huu hakika Allah azza wa jalla amewasifu watu ambao hulala kidogo na kuamka thelusi ya mwisho ya usiku na kuomba maghfira (msamaha) toka kwa Allah, na ewe mja wa Allah hakika ukitaka utukufu mbele ya Allah basi kuwa na kawaida ya kuamka usiku na kufanya ibada, hakika utakuwa miongoni mwa watu watukufu.

Lakini Rasul swalallahu alayh wassalam amesema inafika thelusi ya mwisho ya usiku Allah hushuka katika mbingu ya kwanza na kusema nani anaomba dua nimjibu dua yake, nani ana shida nimtatulie shida yake, nani ana anaomba msamaha nimsamehe madhambi yake.

Je ni nani hana shida? Ni nani hana uhitaji? Na ni nani hana madhambi?

Basi ndugu zangu katika imani faida ya elimu ni kuifanyia kazi,,, lau unaujuzi au ufahamu wa jambo fulani na hulifanyii kazi basi hutofaidika na jambo na hutoona thamani yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…