Ramadhan Special Thread

Mambo Yaliyopendekezwa Kwa Mwenye Kufunga

Imependekezwa kwa mwenye kufunga afuate Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) katika kujitayarisha na swawm yake nayo ni haya yafuatayo;


1. Kula daku
Amehadithia Anas (Radhiya Allaahu ´anhu) Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wasallam) amesema:

‘’Kuleni daku, kwani kula huko daku kuna baraka.” [Imeripotiwa na Imaam Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Nasaa’y na Ibn Maajah].
Na ‘’kuleni daku’’ hata kama kwa kunywa maji inatosheleza. ´Abdullaah Ibn ´Amr amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:

’’Kuleni daku japo kwa kunwa tama la maji.’’

[Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jamiy´ as-Swaghiyr na.2945 imeripotiwa na Ibn Hibbaan].

Pia Imependekezwa kuchelewesha kula daku. Amehadithiya Anas kutoka kwa Zayd ibn Thabit ambaye amesema:

‘’Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) alikula daku kisha akatoka kwenda kuswali. Anas akamuuliza “Kulikuwa na muda gani baina chakula cha daku na adhaana?” Akajibu: “Ilikuwa kiasi cha kusoma Aayah khamsini za Qur-aan".
[Imeripotiwa na Imam Al-Bukhaariy na Muslim].
Pia ameruhusiwa amalize chakula chake anaposikia Adhaana ya Fajr. Abu Hurayrah amehadithia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:

“Endapo mmoja wenu atasikiya adhaana na mkononi mwake ana kinywaji, asirudishe kinywaji hicho mpaka aridhike nacho.

’’[yaani anywe mpaka amalize haja yake]. [Imesahihishwa na Shaykh al-Albaaniy katika al-Jami' as-Swaghiyr na.607].
 
Nikwekua nina uwezo ili jina ningelibadisha kwa kweli nikiona maneno kama hayo naogopa
Nadhani unaongelea jina lako rabii...
Sijui wakati unalitumia ulikuwa na nia gani ama kwa ulimaanisha nini.

Rab'bi maana yake mola mlezi wa viumbe vyote..ni miongoni mwa sifa za mola muumba.
Sifa hii hajapatapo kupewa mwanadamu ama kiumbe chochote pasi na allah mola muumba kwa kuwa yeye ndo mlezi wa viumbe vyote tangu kutungwa kwa mimba hadi kufa.

Allah humuhukumu mtu kutokana na nia yake sidhani kama nia yako ni kujikweza kwa kujipa sifa ya M/Mungu.
Basi M/mungu ni mwingi wa msamaha na atakusamehe inshaaalah

NB.
Lakini pia waweza kuitupa hilo jina na kuja na id mpya hapa utakuwa umetenda jambo jema sana na allah ni mwingi na mbora wa kulipa

Allahu a'alam
 
Rabii ndo jina nililozaliwa nalo nimepewa na wazazi sina a.k.a mimi, ila kwa umri wangu hata nikibadili watu wataniita tu
 
Reactions: SDG
Wa'afua mimkum
 
Sawa mkuu ila kuijua dini ya mwenzako ni vzr sio vibaya kwan unakua kiimani huto yumbishwa
 
Rabii ndo jina nililozaliwa nalo nimepewa na wazazi sina a.k.a mimi, ila kwa umri wangu hata nikibadili watu wataniita tu
Dah basi ni mtihani
Ila kama mtu anataka kumwita mwanae kwa jina linalofanana na hilo basi hana budi kutanguliza neno abdu(mja)...alafu ndo lije jina la allah
Mfano rabii(mlezi) lilitakiwa liwe abdulrabbi(mja wa mlezi) wa viumbe vyote.

Ila ndo hivyo tena ishatokea omba istighfaar na allah ni mwingi wa kusamehe.

NB.
Yes tuwape majina mazuri watoto wetu kama ilivoamrishwa katika dini ila ...
Tuwe makini sana wakati tunawapa watoto wetu majina tuangalie tusijevuka mipaka.

Wallahu aa'lam
 
Ila nia si kujifananisha na mungu ni jina tu
 
Mambo yanayo batikisha swaumu :
# kula na kunywa kwa makusudi
# kujimai(kumuingilia mkeo )mchana wa ramazani
# ukiwa katika siku zako(hii kwa wanawake)
# kujitoa manii kwa Mkusudi

Kuhusu kumuazibu mwanafunzi ambae ni mtuvu wa nizamu hili halikubatilishi swaumu yako
 
Umedokeza kitu muhim sana,usisubiri mtu aulize,wewe ukiwa na muda weka mada hapa ya sala kuanzia udhu na kuendelea.Utakua umeshawasaidia watu na Allah atakulipa.Thread hii ndo mahala pake
 
1.Kula mchana wa ramadhan
2.Kuingiliana kimwili mchana wa ramadhani,hata kama wanandoa
3.Kunywa chochote mchana wa ramadhani.
Kumchapa mwanafunzi hakukuondolei funga,ila jiepushe nako
 
Umedokeza kitu muhim sana,usisubiri mtu aulize,wewe ukiwa na muda weka mada hapa ya sala kuanzia udhu na kuendelea.Utakua umeshawasaidia watu na Allah atakulipa.Thread hii ndo mahala pake
Shukran nitajitahid
 
Reactions: SDG
# mbili sio MKE TU.
Hata hawara hata watu wa JINSI MOJA (MAMBO YAMEBADILIKA SIKU HIZI)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…