Ramadhan Special Thread

Hilo la majina ni mtihani sana, tunaona wakina Karimu walivyojaa, wakina Aziz ndio usiseme, wakina Majid ndio mama weee,

Wengi kuweka ABDU hawaweki sijui ni kusahau au vipi.
 
Hilo la majina ni mtihani sana, tunaona wakina Karimu walivyojaa, wakina Aziz ndio usiseme, wakina Majid ndio mama weee,

Wengi kuweka ABDU hawaweki sijui ni kusahau au vipi.
Na utakuta sisi waswahil ndio wenye tabia ya kukatisha watot wetu majina sijui kwa nin mie sipend kabisa mwanang akatishwe jina lake
 
Enyi waislam wenzangu, napenda kuwakumbusha kuwa tusipende kutoa fat-wa kwa mambo ambayo hatuna uhakika nayo.
Allah anatuambia ktk Qur'an tukufu kwamba:
"Fas-alu ahlu dhikri inkuntum laa ta'alamuun"
Maana yake ni kwamba "waulizeni wenye elimu kwa Yale ambayo hamuyajui"
So ni vyema kufikisha suali ambalo hauna uhakika nalo kwa wenye ujuzi zaidi kabla ya kutoa fat-wa.
Wallah u A'alam!!
 

Wengi humu wananakili fatawa zilizojibiwa na maulamaa kwa munasaba wa maswali hayo hayo. Unless kama kuna kipya amekiingiza au amenukuu jambo pahali pasipo

Allaahu A'aalam
 
Hilo la majina ni mtihani sana, tunaona wakina Karimu walivyojaa, wakina Aziz ndio usiseme, wakina Majid ndio mama weee,

Wengi kuweka ABDU hawaweki sijui ni kusahau au vipi.
Sahihisho.
Unaweza kuita mtoto wako baadhi ya majina ya Mwenyeezi Mungu kutegemea na maana.
Kuna majina mengine maana yake ni sifa ambazo anazo YEYE ALLAH AZZA WA JJALA PEKEYAKE.
Kama Bakii-mwenye kubakia nk.
Lkn Karim ni sifa hata binaadam anaweza kuwa nayo maana yake mkarimu. Au mpole au mwenye huruma. Nk.
Na Allah ndio mwenye kujua zaidi.
 
Labda hizo Rabii ya mwezi mmoja wapo kati ya miezi ya kiarabu.
Rabiiul Awal.
Rabiiul thani. Ama?
Wengine huita rabia
 
Ushauri wangu kwa ndugu zangu ktk Imani ni kuwa, tujitahidi kujipinda na ibada zaidi ktk mwezi huu wa Ramadhan

1. Tuhakikishe tunaswali swala zote kwa wakati bila ya kukosa.

2. Tunajisomea Qur'an kwa wingi na ikiwezekana kumaliza Juzuu 30 zote.

3. Kupata darsa za kuzihuisha nyoyo zetu ili ziweze kudumu na ibada pamoja na kufanya yale yenye kheri

4. Kupata darsa za Tafsiri za Qur'an ili kuweza kutambua maamrisho kama yalivyo ktk Qur'an. Ukishindwa basi Hata kusikiliza Audio kutoka kwa masheikh wetu zinazopatikana ktk web tofauti tofauti kama Alhidaaya, wanachuoni, east africa Quran and Sunna Society. Google ni rafiki muhimu. Ukiweza pia kuna web za kiingereza nitawawekea nikiwa ktk computer.

5. Ramadhan si mfungo wa chakula draft, bali ikiwezekana tuwatafute wasio na uwezo tuwape sadaka ya vyakula ambavyo wengi wetu hufanya israfu.

6. Taraweh na Sala za usiku ziwe katika malengo yetu na hakikisha unahudhuria misikiti ambayo ina visomo virefu ili ku maximize muda wetu kwenye ibada.

7. Tujiepushe na laghwi zozote. Mfano frequenting ktk websites za kuchat tu, miziki na mengineyo yasiyomfurahisha Muumba. Games kwa munasaba wa kupoteza muda si mahala muafaka ktk Ramadhan bali yatupasa tuipambe ramadha kwa Nyiradi, visomo na kusikiliza Quran.

8. Tuombe maghf'iraa kwa wingi sana, ikiwezekana lia na nafsi yako, toa machozi kujisuta kwa madhambi tuliyowahi kuyafanya na tuazimie kutorejea tena ktk madhambi hayo mfano wa Riba, utesi, zinaa, wizi, kusengenya, shiriki, kula mali za yatima, dhulma, liwatwi, kuacha kusali, kuacha kuhiji kwa wenye uwezo na mengi ktk madhambi ambayo Iblis mwenye laana ametupambia nayo.

9. Tuunge udugu kwa kutembeleana na kufuturishana.

10. Tutoleane salamu na tujiweke mbali na mikusanyiko ambayo kwayo maasia yanapatikana.

Allaah atufanyie wepesi sote na tuiombee nchi yetu na viongozi wetu ili Wasiipoteze hii nchi na kuiharibu.

Ameen

 
Kumeibuka wimbi kubwa la vijana ambao hawatak kufunga, kwa kujitia visingizio mbali mbali ikiwemo maradhi hasa vidonda vya tumbo.
Hivyo bac nawaasa vijana wa kiislam fungeni jamani, kuna hadith ya mtume iliyopokelewa na Imam Muslim inasema:
"Swumuu taswiih"
Ikiwa na maana;
"Fungeni mtapata afya"
Hii imethibitishwa na wanasayansi wa karne hizi na kuprove maneno haya ya mtume kwamba funga ina faida kubwa kwa afya ya mfungaji.
Wabillah ttawfiiq.
 
Na utakuta sisi waswahil ndio wenye tabia ya kukatisha watot wetu majina sijui kwa nin mie sipend kabisa mwanang akatishwe jina lake
Ramadhani aka Ramsey, aka Ramso [emoji735][emoji735][emoji735]
 
Mambo yote muhimu [emoji115]
 
KUFUNGA SI KUACHA KULA TU NA KUNYWA Bali pia,
1)kujiepusha na kauli chafu.
2)kujiepusha kuangalia machafu
3)kujiepusha na kusengenya
4)kujiepusha na kusema uongo
Kujiepusha na yote hayo kwa maana ili funga zetu zisiwe n shaqqa ndani yake
....
Ni vizuri zaid kusoma Quran kwa sana ktk mwez huu ,kufanya istighfar kwa sana,kufanya ibada ipasavo na min waqt
Allah anajua zaidi.
Shukran.
 
Nimekutafuta wee angalau nikudokeze uje huku upate mawili matatu ila sijakuona.

Karibu my kwa lolote lenye faida kuhusu mwezi wetu Mtukufu wa ramadhan sio mbaya ukaliweka humu tukazidi kupata elimu zaidi.
Asante sn my,ndio Kwanza naona Sasa huu uzi.
Tuko pmj insha Allah[emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…