Hakika matendo bora kabisa ni yale ya mwisho,na hata ramadhani hii ubora wake hasa huja mwishoni na ndio maana hata usiku wa laila tul qadir inasemwa umewekwa katika kumi la mwisho
Ndugu zangu kwakujua hilo kipenzi chetu Muhammad swalla llahu alaihy wassalaam alikuwa anapenda kuomba dua hii katika uhai wake,nasi ni bora tutakidhirisha kuiomba sana dua hii
"Ewe Allah ufanye umri wangu uwe bora zaidi katika mwisho wake,uyafanye matendo yangu yawe bora zaidi katika mwisho wake na uifanye siku yangu ya mwisho bora ni siku nikakayo kutana na wewe"
Inasemwa hutokea mtu akafanya matendo mazuri sana katika umri wake kisha ikabakia ridhaa moja au mbili kuifikia pepo kisha akafanya matendo ya watu wa motoni na kisha kuingia motoni
Inasemwa mtu hutokea akafanya matendo mabaya katika umri wake wote,kisha ikabakia ridhaa moja au mbili kufikia motoni kisha akafanya matendo ya watu wa peponi kisha akaingi peponi
Dua hiyo ya Mtume inaonyesha umuhimu wa kuomba mwisho mwema,kwahiyo tusiache sana kumuomba Allah atupe mwisho mwema
Katika miongoni mwa vita za jihadi,kuna mtu mtu mmoja alikuwa anapigana kwa juhudi kubwa sana katika njia ya Allah,mpaka wakasema mtu huyu ataingia peponi,lkn Mtume alivyowasikia akasema mtu huyu ataingia motoni
Hakika wakiwa uwanja wa vita,masahaba hawakumuelewa kabisa mtume,inakuwaje mtu huyu tunae hapa anapigana katika njia ya Allah na kisha isemwe ataingia motonii,kwakweli iliwasumbua kidogo hii kauli ya rasul
Kama inavyojulikana Mtume swalla llahu alaihy wa salaam hasemi kwa matamanio yake bali huwa ni maono au wahyi toka kwa Allah,basi mwisho wa siku yule mtu kutokana na majeraha aliyoyapata akashindwa kuvumilia maumivu na mwisho wa siku akajiua
Hapo sasa ndio masahaba wakazinduka kutoka usingizini na kukumbuka kauli ya rasul juu ya mtu huyo kuingia motoni
Kumbuka mwisho bora wa matendo yetu ni ya mwisho kabisa,haijalishi ulifanya dhambi gani kubwa,tubadilike na tuazimie kuwa na mwisho mwema na tuombe sana kwa Allah atupe mwisho mwema