Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

IMG_20250308_171906.jpg
 
Inasikitisha sana watu baada ya kufuturu wanaingiwa na uvivu wa kuswali swala ya faradhi ya isha,na hata tarawehee ambayo ni sunna muhimu sana miongoni mwa swala za usiku

Huu ni mwezi wa kuchuma sasa mbona hatuitumii hii fursa?
 
Wenzetu maswahaba walipokuwa wanaagana baada ya mazungumzo yao,walikuwa wanapeana nasaha kwa kusomeana suratil al asir ndio kisha wanaagana

Sura hii inazungumzia kwamba hakika wanadamu wote haijalishi waislamu au wasio waislamu,kuanzia baba yetu Adamu mpaka Mtume wa mwisho Muhammad swalla lahhu alaihy wa salaam, wote wapo katika hasara

Isipokuwa wale waliomwamini Allah kwa maana Mungu mmoja, kisha wakafanya mambo mema kwa maana matendo mema,kisha wakahusiana kuhusu mambo ya haki,kwa maana haki ya kumjua Allah, kukijua kitabu cha Allah na kujua mafundisho sahihi ya mtume Muhammad

Kisha wakahusiana juu ya kusubiri,hakika subira ni ibada kubwa sana,maana uwe na subira ya kuacha maovu uliyoyazoea na uwe na subira na kudumu kufanya mambo mema,maana hakika kudumu kufanya ibada za Allah ni mtihani mkubwa sana

Hawa ndio ambao hawapo katika hasara yani wamesamilika

Je sisi tupo upande upi? Tujitathimini na kufanya yale yenye kutupa mwisho mwema
 
Siku ya jana nikiwa pale mloganzila nimempeleka mzee wangu katika clinic yake,katika korido za pale hospitalini nikamsikia muislamu mwenzangu anaongea na simu huku akisema " tutamuoshea hapa hapa na kumswalia kabisa huku huku"

Naam huyo ni ndugu yetu katika imani ameondoka jana katika mgongo wa ardhi,na huenda yeye na wengine kama yeye waliazima kumaliza mfungo salama lkn hakika umri wao wa kuishi duniani umefikia mwisho


Je mimi na wewe ambao tupo hai hadi leo tunajitahidi vipi kuchuma zaidi ndani ya mwezi huu,je tutafanikiwa kumaliza salama mfungo au nasi huenda ikatufika safar ya kwenda kwa mola wetu?

Tutumie kila dakika na sekunde ya uhai wetu katika mwezi huu kuchuma thawabu nyingi zaidi kwani huenda,tusiimalize ramadhani hii au ama tusikutane na ramadhani nyengine

Tumche Allah sana
 
Katika suratil al asiri Allah ameapa kwa wakati,hakika wakati ni rasimali muhumu sana katika maisha ya mwanadamu,kwahiyo usiutumie wakati wako vibaya hata kidogo hasa katika mwezi huu wa ramadhani

Utamsikia mtu anasema ngoja niende kijiweni nikapoteze wakati hakika ni msiba mkubwa,huu ni wakati wa kufanya amali nyingi zaidi,sikiliza darsa na mawaidha ya dini,soma qur'an,fanya dhikri utajo wa Allah kwa wingi na yale yote ambayo yatakuongezea akaunti ya mema yako

Masiku yenyewe ni machache mno kama anavyosema Allah subhana wa taala,basi ndugu zangu katika imani huu si wakati wa kupoteza mda kuangalia filamu na series mbali mbali,bali ni wakati wa kufanya amali zaidi kadri iweze kanavyo ili tufaidike na mwezi huu

Mtume Muhammad swalla llahu alaihy wasalaam,anasema hakika amepata khasara yule ambaye ramadhani imemfikia na kisha asisamehewe na Allah
 
Hakika matendo bora kabisa ni yale ya mwisho,na hata ramadhani hii ubora wake hasa huja mwishoni na ndio maana hata usiku wa laila tul qadir inasemwa umewekwa katika kumi la mwisho

Ndugu zangu kwakujua hilo kipenzi chetu Muhammad swalla llahu alaihy wassalaam alikuwa anapenda kuomba dua hii katika uhai wake,nasi ni bora tutakidhirisha kuiomba sana dua hii

"Ewe Allah ufanye umri wangu uwe bora zaidi katika mwisho wake,uyafanye matendo yangu yawe bora zaidi katika mwisho wake na uifanye siku yangu ya mwisho bora ni siku nikakayo kutana na wewe"

Inasemwa hutokea mtu akafanya matendo mazuri sana katika umri wake kisha ikabakia ridhaa moja au mbili kuifikia pepo kisha akafanya matendo ya watu wa motoni na kisha kuingia motoni

Inasemwa mtu hutokea akafanya matendo mabaya katika umri wake wote,kisha ikabakia ridhaa moja au mbili kufikia motoni kisha akafanya matendo ya watu wa peponi kisha akaingi peponi

Dua hiyo ya Mtume inaonyesha umuhimu wa kuomba mwisho mwema,kwahiyo tusiache sana kumuomba Allah atupe mwisho mwema

Katika miongoni mwa vita za jihadi,kuna mtu mtu mmoja alikuwa anapigana kwa juhudi kubwa sana katika njia ya Allah,mpaka wakasema mtu huyu ataingia peponi,lkn Mtume alivyowasikia akasema mtu huyu ataingia motoni

Hakika wakiwa uwanja wa vita,masahaba hawakumuelewa kabisa mtume,inakuwaje mtu huyu tunae hapa anapigana katika njia ya Allah na kisha isemwe ataingia motonii,kwakweli iliwasumbua kidogo hii kauli ya rasul

Kama inavyojulikana Mtume swalla llahu alaihy wa salaam hasemi kwa matamanio yake bali huwa ni maono au wahyi toka kwa Allah,basi mwisho wa siku yule mtu kutokana na majeraha aliyoyapata akashindwa kuvumilia maumivu na mwisho wa siku akajiua

Hapo sasa ndio masahaba wakazinduka kutoka usingizini na kukumbuka kauli ya rasul juu ya mtu huyo kuingia motoni

Kumbuka mwisho bora wa matendo yetu ni ya mwisho kabisa,haijalishi ulifanya dhambi gani kubwa,tubadilike na tuazimie kuwa na mwisho mwema na tuombe sana kwa Allah atupe mwisho mwema
 
Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake,anasema akitaka mtu daftar lake la matendo limfurahishe siku ya kiama au siku ya hesabu basi apende sana kuomba msamaha kwa kusema astaghfirullah mara kwa mara

Na ndio maana dua bora sana kudumu nayo na ambayo pia ni dhikri nzur kuifanya mwezi huu wa ramadhani ni "Allahuma innaka afuwun tuhibulah afwa fafuana"

Ewe mola wangu hakika wewe ni msamehevu na unapenda kusamehe basi nisamehe

Tumche Allah ukweli wa kumcha
 
Back
Top Bottom