Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Kwa kweli sijui ni kiongozi yupi anaeongoza dunia kwa sasa.ila rank ya uongozi ipo inaanza na mtume,maswahaba zake,maimamu wanne...baada ya hapo sifaham

Kuhusu nani afuturishwe sina elimu nalo la ushahidi wa aya au Quran
Ila tumeusiwa kuwakumbuka sana mayatima na maskini kwenye maisha yetu.
Kulingana na taratibu na matakwa ya sheria,kwa sasa hakuna kiongozi wa waislamu wote duniani. Tangu kuanguka dola ya Uthmaan hakujasimama khilafa nyingine.

Kufuturisha ni kwa kila aliyefunga. Anayejitahidi kwa ibada ni bora zaidi
 
Kwa wale wanaosingizia vidonda vya tumbo tumuogope Allah, kwani siku 30 ni kidogo sana, vipi lakini hukumu ya wale wanaoumwa kweli vidonda vya tumbo?
Kwa yeyote ambaye hatafunga kwa ajili ya maradhi wakati wa mwezi ramadhani, atakula mchana wa ramadhani ila atatakiwa kulipa baada tu ya eid na asiikutanishe swaumu hiyo na ramadhani nyingine.

Ama kwa mwenye maradhi ya kudumu kama vidonda vya tumbo, kisukari nk. Atakula mchana wa ramadhani (ale kistaarabu, asile hadaharani kwa sifa) na kwa kila siku ambayo hajafunga basi atatoa kibaba kimoja cha chakula kinachopendwa zaidi katika mji kumfuturisha maskini.

Pia kuna hukumu ya mama mjazito au mama anayenyonyesha mtoto mchanga, nitaendelea baadae in shaa allah.

Ama kwa yule ambaye ataacha kufunga kwa makusudi bila udhuru wa kisheria, anapata madhambi na anajitoa miongoni mwa walioamini kwani funga ni lazima kwa wale walioamini na allah atawalipa kadri ya makosa yao.
Wallahu A'lam
 
Nawausia waislam na wale ambao sio waislam tuepuke sana zinaa, inasikitisha sana kuona mtu ameoa afu tena anzini
 
cfb105bf4be271902d6a60b4899c908a.jpg


Kina dada Acheni Usanii Mwezi wa Ramadhani
 
Huwezi amini kwa hizi avatar zetu jamani, mtu kama;

1. Hence mtanashati
2.byong
3.thatsist

Ni miongoni mwa waislam wazuri kabisa ivi kwenye dini yao, Allah atujalie mwisho mwema, wenye nia ya hijah Allah atujalie sote kwenda kuiona alkaba.

Hongera kwa
1.Emmyta
2. Uhuhty ( kama sijakosea), najua wanaijua dini yao.

Tumkaribishe Dada yetu mpendwa bi. Faizafoxy
FaizaFoxy wapotozee hao ccm kwa mda dimaa anakuomba uje japo kusalimia pande hizi, watu wanachuma matunda ya peponi huku
 
Huwezi amini kwa hizi avatar zetu jamani, mtu kama;

1. Hence mtanashati
2.byong
3.thatsist

Ni miongoni mwa waislam wazuri kabisa ivi kwenye dini yao, Allah atujalie mwisho mwema, wenye nia ya hijah Allah atujalie sote kwenda kuiona alkaba.

Hongera kwa
1.Emmyta
2. Uhuhty ( kama sijakosea), najua wanaijua dini yao.

Tumkaribishe Dada yetu mpendwa bi. Faizafoxy
Faiza Foxy sijui kapolea wapi
 
Back
Top Bottom