Ramadhan Special Thread

kila la heri kwa ndugu zetu,
ila ni vyema kwa kina dada wavae mavazi yenye heshima muda wote hata baada ya mfungo. ni unafiki mkubwa kujifanya unaheshimu mwezi huu halafu badae unaendeleza uhuni wako.
 
Kulingana na taratibu na matakwa ya sheria,kwa sasa hakuna kiongozi wa waislamu wote duniani. Tangu kuanguka dola ya Uthmaan hakujasimama khilafa nyingine.

Kufuturisha ni kwa kila aliyefunga. Anayejitahidi kwa ibada ni bora zaidi
 
Kwa wale wanaosingizia vidonda vya tumbo tumuogope Allah, kwani siku 30 ni kidogo sana, vipi lakini hukumu ya wale wanaoumwa kweli vidonda vya tumbo?
Kwa yeyote ambaye hatafunga kwa ajili ya maradhi wakati wa mwezi ramadhani, atakula mchana wa ramadhani ila atatakiwa kulipa baada tu ya eid na asiikutanishe swaumu hiyo na ramadhani nyingine.

Ama kwa mwenye maradhi ya kudumu kama vidonda vya tumbo, kisukari nk. Atakula mchana wa ramadhani (ale kistaarabu, asile hadaharani kwa sifa) na kwa kila siku ambayo hajafunga basi atatoa kibaba kimoja cha chakula kinachopendwa zaidi katika mji kumfuturisha maskini.

Pia kuna hukumu ya mama mjazito au mama anayenyonyesha mtoto mchanga, nitaendelea baadae in shaa allah.

Ama kwa yule ambaye ataacha kufunga kwa makusudi bila udhuru wa kisheria, anapata madhambi na anajitoa miongoni mwa walioamini kwani funga ni lazima kwa wale walioamini na allah atawalipa kadri ya makosa yao.
Wallahu A'lam
 
Nawausia waislam na wale ambao sio waislam tuepuke sana zinaa, inasikitisha sana kuona mtu ameoa afu tena anzini
 
FaizaFoxy wapotozee hao ccm kwa mda dimaa anakuomba uje japo kusalimia pande hizi, watu wanachuma matunda ya peponi huku
 
Faiza Foxy sijui kapolea wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…