Ramadhan Special Thread

Hata haipendezi unapokuja kwa fujo kwenye jambo ambalo hata wewe hulifanyi.

Ndio mana ikaitwa imani wacha mwenye kuamini aamini hivyo. Sio lengo la huu uzi kukashifiana.

Jaribu kustaarabika ni ombi sio lazima lakini.
Posti kama ya huyo jamaa huna hata haja ya kuijibu. Watu kama hao walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo. Usiumize kichwa dada.
 
Tusiruhusu na tusikubali vitu vya sunnah vitugawe au kuchukiana waislam, ufunge mwezi wa kimataifa ama kitaifa sote njia yetu ni moja. Mtume mwenyewe kashatuambia kwamba wakh- tillaf ummat rehmaat ( kugawanyika kwa umma wangu ni rehmaa), allah atujalie pepo.
 
Sasa msiwe waislam wa ramadhAn tu mnk nina jamaa angu yeye anafunga vzr akifuturi anarud kwenye fegi
 


Kalenda ya kiislamu ilianza mwaka 622AD
Huo ni mwaka wa kihistoria wa kiislamu ambapo Mtume(s.a.w.) alihama kutoka maka kwenda madina
Kalenda ya kiislamu ina miezi 12
1. Muharram (mfungo 4)
2.Safar
3.Rabi-ul Awwal (mfungo 6)
4.Rabi –ul-Akhir
5.Jumaada –ul Awwal
6.Jumaada ul Akhir
7.Rajab
8.Shaaban
9.Ramadhan
10.Shawwal
11.Dhul Qaadah (mfungo 2 )
12. Dhul Hijja (mfungo 3 )

KANUNI NZURI YA KUJUA MWAKA WA KIISLAMU/WA KIMATAIFA TUMIA HII
G = (32H : 33) + 622
M = {33*(K - 622)): 32
G=INTERNATIONAL CALENDAR
M=ISLAM CALENDAR


BAADHI YA MATUKIO MUHIMU YA KIHISTORIAKATIKA UISLAM
496 AD Alizaliwa babu yake Mtume (s.a.w ) Bwana Abdul Muttalib
545 AD Alizaliwa baba yake Mtume (s.a.w )-Abdillah Bin Abdul Muttalib
546 AD Alizaliwa mama yake Mtume (s.a.w )-Bi Amina Bint Wahab
571 AD Alizaliwa Muhammad Bin Abdillah (s.a.w) (mfungo 6 )
576 AD Alikufa mama yake Mtume (s.a.w)
578 AD Alikufa babu yake Mtume (s.a.w )
595 AD Mtume (s.a.w) aliamuoa Bi khadija (r.a)
610 AD Alishushiwa utume (sawa na mwezi 17 Ramadhan )
613 AD Alizaliwa Bi Aisha Bint Abubakar (r.a)
616 AD Alisilimu Sayyidina Umar (r.a)
620 AD Walifariki Bi khadija (r.a) na Bwana Abu Talib
621 AD Safari ya miraji ya Mtume (s.a.w) na kufaradhishwa sala 5 (mwezi wa Rajab)
622 AD Hijra ya Mtume(s.a.w) pamoja na masahaba
623 AD=2AH Aliolewa Bi Aisha (r.a ) na Mtume (s.aw.) pia ndiyo mwaka iliofaradhishwa Ramadhan na kutoa Zaka
628 AD=7AH Ilifaradhishwa Hijja
632 AD=11AH Alikufa Mtume(s.aw) na mwaka huo miezi 6 baadae alikuja kufa Binti yake kipenzi Fatma (r.a)
677AD=57AH Alifariki mke kipenzi wa Mtume Aisha (r.a)
haya ni baadhi tu miongoni mwa matukio mengi makubwa yaliotokea katika historia ya uislam
NB.
AD=After Death
AH=After Hijra







 
Shukran
 
Ndugu zangu katika imani!

Leo mimi na wewe tunajivunia kuitwa waislamu ila tusisahau hii dini wenzetu wameitoa mbali

mwaka 622AD ni mwaka uliokuwa muhimu mno katika ustawi wa dini yetu, masahaba waliacha mali zao, familia zao na ardhi yao wakaondoka/hijra ili wailinde imani yao na wapate radhi za M/Mungu (s.w) na hii yote ni katika kudra zake na mapenzi yake M/Mungu (s.w.) kwani akitaka dunia nzima anaweza akaishuritisha tukawa waislamu, lakini hajaruhusu hilo ili apime imani zetu

''je mnadhani mtaingia peponi hali ya kuwa hayajawapata mfano wa yale yaliowapata wale waliokuwa kabla yenu,iliwapata shida na madhara wakatikiswa hata Mtume na walioamini wakasema:hivi nusra ya Mwenyezi Mungu itakuja lini........??'' (Q:2:214)

Na sisi tunaomfata Mtume (s.aw) na masahaba yatakiwa tufanyae hijra, na hijra yetu katika zama zetu hizi zilizojaa watu wa imani haba,ni kuyakimbia maasi
Ikiwa kuna mambo hayampendezi Mungu tunayafanya, ni wakati sasa nasi tufanye hijra tuyakimbie ili tupate radhi za M/Mungu (s.w)
 

Ahsante sana dimaa, nimekaribia.

Ya Raab tunakuomba mtakabalie dimaa dua yake njema. Amin.

Ramadhan Kareem.
 
Kuna kitu nimekumbuka; kuna uzi nimemjibu Mkenya hapa: Kwa wadau wote wa jamii forums

Baada ya kuujibu huo uzi nikaukumbuka uzi huu mwema ulioanzishwa na Hance Mtanashati, ukisoma maudhui ya huyo Mkenya na ukisoma nilichomjibu nawaombeni wote mnaopitia uzi huu muwaunge mkono Bi Zainab Tamim na mumewe kwa juhudi zao za kujitolea kuanzisha, kuunda na kutuletea kitu chema sana ambacho binafsi nnaamini ni cha manufaa kwa wote.

Jisomee: Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

Nnafuraha kubwa kusema kuwa binafsi ni kati ya watu 50 wa mwanzo kujiunga.

Ramadhan Kareem.
 
Hadithi hiyo ya kugawanyika umma kuwa ni rahma sio sahihi. Ni maudhwuuu(uongo).
Kwani kinyume chake itakuwa 'ijtimaai ummatii naqma'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…