ukhuty
JF-Expert Member
- Oct 9, 2016
- 16,879
- 41,971
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Posti kama ya huyo jamaa huna hata haja ya kuijibu. Watu kama hao walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo. Usiumize kichwa dada.Hata haipendezi unapokuja kwa fujo kwenye jambo ambalo hata wewe hulifanyi.
Ndio mana ikaitwa imani wacha mwenye kuamini aamini hivyo. Sio lengo la huu uzi kukashifiana.
Jaribu kustaarabika ni ombi sio lazima lakini.
Jitahd miss,sijui kama funga yangu itakuwa inafika hata saa nne asubuhi .tumbo hili litanipeleka motoni mimi
Alshabaab sio diniNasikia wale Al shabaab wanasemaga ni haram mwislamu kutumia internet ni kweli? Maana wao wenyewe wana account hadi Twitter.
ShukranView attachment 514503
Kalenda ya kiislamu ilianza mwaka 622AD
Huo ni mwaka wa kihistoria wa kiislamu ambapo Mtume(s.a.w.) alihama kutoka maka kwenda madina
Kalenda ya kiislamu ina miezi 12
1. Muharram (mfungo 4)
2.Safar
3.Rabi-ul Awwal (mfungo 6)
4.Rabi –ul-Akhir
5.Jumaada –ul Awwal
6.Jumaada ul Akhir
7.Rajab
8.Shaaban
9.Ramadhan
10.Shawwal
11.Dhul Qaadah (mfungo 2 )
12. Dhul Hijja (mfungo 3 )
KANUNI NZURI YA KUJUA MWAKA WA KIISLAMU/WA KIMATAIFA TUMIA HII
G = (32H : 33) + 622
M = {33*(K - 622)): 32
G=INTERNATIONAL CALENDAR
M=ISLAM CALENDAR
BAADHI YA MATUKIO MUHIMU YA KIHISTORIAKATIKA UISLAM
496 AD Alizaliwa babu yake Mtume (s.a.w ) Bwana Abdul Muttalib
545 AD Alizaliwa baba yake Mtume (s.a.w )-Abdillah Bin Abdul Muttalib
546 AD Alizaliwa mama yake Mtume (s.a.w )-Bi Amina Bint Wahab
571 AD Alizaliwa Muhammad Bin Abdillah (s.a.w) (mfungo 6 )
576 AD Alikufa mama yake Mtume (s.a.w)
578 AD Alikufa babu yake Mtume (s.a.w )
595 AD Mtume (s.a.w) aliamuoa Bi khadija (r.a)
610 AD Alishushiwa utume (sawa na mwezi 17 Ramadhan )
613 AD Alizaliwa Bi Aisha Bint Abubakar (r.a)
616 AD Alisilimu Sayyidina Umar (r.a)
620 AD Walifariki Bi khadija (r.a) na Bwana Abu Talib
621 AD Safari ya miraji ya Mtume (s.a.w) na kufaradhishwa sala 5 (mwezi wa Rajab)
622 AD Hijra ya Mtume(s.a.w) pamoja na masahaba
623 AD=2AH Aliolewa Bi Aisha (r.a ) na Mtume (s.aw.) pia ndiyo mwaka iliofaradhishwa Ramadhan na kutoa Zaka
628 AD=7AH Ilifaradhishwa Hijja
632 AD=11AH Alikufa Mtume(s.aw) na mwaka huo miezi 6 baadae alikuja kufa Binti yake kipenzi Fatma (r.a)
677AD=57AH Alifariki mke kipenzi wa Mtume Aisha (r.a)
haya ni baadhi tu miongoni mwa matukio mengi makubwa yaliotokea katika historia ya uislam
NB.
AD=After Death
AH=After Hijra
Shukran ukhty faizaMa sha Allah Tabaraka Allah.
Ramadhan njema kwa wote.
Huwezi amini kwa hizi avatar zetu jamani, mtu kama;
1. Hence mtanashati
2.byong
3.thatsist
Ni miongoni mwa waislam wazuri kabisa ivi kwenye dini yao, Allah atujalie mwisho mwema, wenye nia ya hijah Allah atujalie sote kwenda kuiona alkaba.
Hongera kwa
1.Emmyta
2. Uhuhty ( kama sijakosea), najua wanaijua dini yao.
Tumkaribishe Dada yetu mpendwa bi. Faizafoxy
Hadithi hiyo ya kugawanyika umma kuwa ni rahma sio sahihi. Ni maudhwuuu(uongo).Tusiruhusu na tusikubali vitu vya sunnah vitugawe au kuchukiana waislam, ufunge mwezi wa kimataifa ama kitaifa sote njia yetu ni moja. Mtume mwenyewe kashatuambia kwamba wakh- tillaf ummat rehmaat ( kugawanyika kwa umma wangu ni rehmaa), allah atujalie pepo.
sijui kama funga yangu itakuwa inafika hata saa nne asubuhi .tumbo hili litanipeleka motoni mimi