masharti ya swalah
Masharti ya swalah ni tisa:
Sharti ya kwanza: Uislamu.
Sharti ya pili: Mtu kuwa na akili.
Sharti ya tatu: Uwezo wa kupambanua.
Sharti ya nne: Kuondosha hadathi.
Sharti ya tano: Kuondosha najisi.
Sharti ya sita: Kufunika zile sehemu zisizotakiwa kuonekana (´Awrah).
Sharti ya saba: Kuingia kwa wakati.
Sharti ya nane: Kuelekea Qiblah.
Sharti ya tisa: Kunuia.
Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Chanzo: Duruus-ul-Muhimmah li ´Aammah al-Ummah, uk. 12
Tarjama: Wanachuoni.com
nguzo za swalah
Nguzo za swalah ni kumi na nne:
Nguzo ya kwanza: Kusimama kwa mwenye kuweza.
Nguzo ya pili: Kusema "Allaahu Akabr".
Nguzo ya tatu: Kusoma Suurah "al-Faatihah."
Nguzo ya nne: Kurukuu.
Nguzo ya tano: Kuinuka kwenye Rukuu´.
Nguzo ya sita: Kusujudu juu ya viungo saba.
Nguzo ya saba: Kutoka hapo.
Nguzo ya nane: Kukaa baina ya Sajdah mbili.
Nguzo ya tisa: Kuwa na utulivu katika nguzo zote.
Nguzo ya kumi: Kuzipangilia.
Nguzo ya kumi na moja: Tashahhud ya mwisho.
Nguzo ya kumi na mbili: Kukaa katika [Tashahhud] hiyo.
Nguzo ya kumi na tatu: Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Nguzo ya kumi na nne: Kuleta Tasliym mbili.
Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Chanzo: Duruus-ul-Muhimmah li ´Aammah al-Ummah, uk. 13
Tarjama: Wanachuoni.com
mambo ya wajibu ya swalah
Mambo ya wajibu ya swalah ya ni manane:
La kwanza: Kusema "Allaahu Akbar" mbali na ile ya kwanza.
La pili: Kusema "Sami´ Allaahu li man hamidah" kwa imamu na anayeswali peke yake.
La tatu: Kusema "Rabbanaa wa lak al-Hamd". Inasemwa na wote.
La nne: Kusema "Subhaana Rabbiy al-´Adhwiym" katika Rukuu´.
La tano: Kusema "Subhaana Rabbiy´ al-A´laa" katika Sujuud.
La sita: Kusema "Rabb Ighfir liy" kati ya Sajdah mbili.
La saba na la nane: Tashahhud ya kwanza na kukaa kwayo.
Mwandishi: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Chanzo: Duruus-ul-Muhimmah li ´Aammah al-Ummah, uk. 13-14
Tarjama: Wanachuoni.com