Hance Mtanashati allah akulipe kheri kwa kuanzisha uzi huu na ramadhan itufanye ste kubadilika kushika njia yake ameeen
JazakAllah khayrSWALI :
Asalaam alaykum.
Napenda kuuliza suala langu kuhusu Ramadhan "Nimeamka usiku na kula daku mapema, lakini nikaamka usiku na kuendelea na ibada, nilipokuwa nikiendelea na ibada, mara kiu ikanishika na nikanywa maji, lakini kwa bahati nikasikia adhana ya pili ya sala ya alfajiri, wakati huu, yale maji nusu yamekwenda na nusu yamo mdomoni, nikaendelea kuyanywa yale yaliyo mdomoni wakati huu adhana hiyo ya pili inaendelea kusomwa. JEE HUKUMU YANGU NINI KUHUSU USAHIHI WA FUNGA YANGU
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
“…Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku...” Al-Baqarah: 187
Ni waajib kwa mwenye kufunga ajizuie kula au kunywa pale panapoingia Alfajiri ya kweli, kwa hali ya leo hii wengi wanajua alfajiri ya kweli kwa sauti ya Adhaan ya pili japo hiyo inaweza isiwe ni kipimo sahihi mia kwa mia kwani Misikiti mingi huadhiniwa kwa kutazamwa saa na si kwa kutazamwa weupe wa alfajiri ya kweli kama ushadhihirika au la.
Swawm yako inaweza kuwa ni sahihi kutokana na kutokujua kwako hukumu ya jambo hilo.
Hadiyth ifuatayo inatuonyesha kuwa mtu anaruhusiwa kumaliza tonge au chakula chake alichoonza kula wakati Adhaan inapoadhiniwa:
Imesimuliwa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):“Atakaposikia mmoja wenu Adhaan na hali ana chombo cha chakula mkononi mwake, asikishushe chini hadi amalize kilichomo”[Ahmad, Abu Daawuud, na Shaykh Al-Albaaniy kaitaja katika Swahiyh ya Abu Daawuud].
Hata hivyo, Hadiyth hii isichukuliwe moja kwa moja kuwa mtu anaweza kuendelea kula na hali ishaingia Alfajiri ya kweli. Kwani kuna makatazo ya wazi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:
“Msisimamishe daku yenu mnaposikia Adhaan ya Bilaal, kwani yeye anaadhini usiku, kwa hiyo kuleni na kunyweni mpaka Ibn Umm Maktuum aadhini.” Al-Bukhaariy
Kwa hali yako muulizaji, ni bora uwe makini kutokula tena baada ya Adhaan ya pili ambayo huwa ndio kipimo cha Alfajiri ya kweli, na kwa sababu ulikuwa hujui hukumu hapo mwanzo, basi tunataraji Swawm yako itakuwa sahihi inshaAllaah.
Lakini ni vizuri Muislamu kuchukua tahadhari ya kujua muda gani khaswa Adhaan ya kwanza na muda gani ni Adhaan ya pili ili asalimike na matukio kama haya. Hakika ni dakika chache tu mtu unaweza kujiweka katika usalama wa kula daku
shukrani mkuuMwezi wa Ramadan unaagiza watu kufanya mema mambo mazuri yanayo mpendeza Mungu ivyo kwa kuwa Mungu wetu ni Baba wa mambo mema basi hata sisi wa kristo tuna heshimu mwezi huu wa Ramadhan kwa kutenda mambo mema
Mfano mm mwezi huu wote natulia kwa kutenda mambo mema na kuacha mambo maovu kama zinaa na mengine
By Pastor Askari Muoga
Swadakta mkuu[emoji184]السؤال Swali
ما حكم الصوم مع ترك الصلاة في رمضان؟
Nini hukumu ya funga ya mtu asiyeswali?
[emoji430]فأجاب الشيخ بن عثيمين رحمه الله:
Akajibu Shekh Bin Uthaimin Allah amrehem
إن الذي يصوم ولا يصلي لا ينفعه صيامه Hakika yule ambaye anafunga na wala haswali hainufaishi funga
yake
ولا يُقْبَل منه ولا تبرَأ به ذمَّته.
Wala haikubaliki kwake hiyo funga na wala haimuondoi yeye kwenye dhima ya kutekeleza hiyo funga(anahesabika kuwa hajafunga)
بل إنه ليس مطالباً به مادام لا يصلي؛
Bali hakika ya hiyo funga yake haihitajiki maadam haswai
لأن الذي لا يصلي مثل اليهودي والنصراني،
Kwasababu asiyeswali ni mfano wa Myahudi na Mnaswara
فما رأيكم أن يهوديًّا أو نصرانيًّا صام وهو على دينه، فهل يقبل منه؟
Mnaonaje iwapo Myahudi au Mnaswara akifunga na hali yuko kwenye dini yake, Je atakubaliwa funga yake?
لا. إذن نقول لهذا الشخص:
Hapana, haiwezi kukubaliwa, kwahiyo tunasema kumwambia huyu mtu:
تب إلى الله بالصلاة وصم،
Tubia kwa Allah, kwa kuswali na kufunga.
ومَن تاب تاب الله عليه.
Na atakayetubu, Allaah atamkubalia toba yake
والله{سبحنه وتعلا} اعلم.
Pepo nyepesi sana ukifata kwa ukamilifu Qur-an na Sunnah za Mtume (S.A.W)duuu pepo ngumu sana
Allah haibadilishi nafsi ya mja mpaka wewe mwenyewe uibadilishe nafsi yako..Wajamvi habarini
Kifupi nmejitahid kupigana na hii hali kwa muda mrefu sasa lakini kwa neema za mungu nauona huu mwezi nataka niache kabisa uzinzi na punyeto
Mungu nisaidie
Yyah vizur aisee.Ni kweli asee, hasahasa Facebook na instagram, Mimi hiyo nishaisahau hata kama nimitandao ya kijamii, natumiaga whatsap pekee