Ramadhan Special Thread

Mkuu ukipata mda, endelea kutuletea zaidi hizi mada za swala
Mungu akulipe kheri
 
Ebwana waungwana kwenye hii thread kuna anayefuturisha??
 
Masha Allah. Ukumbusho mzuri sana huu na wenye manufaa.
Allah Atuwafikishe yarab.
Ameen

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
ASSALAM ALAYKUM WARAHMATULLAHI WABARAKATUH.

Ninachukua fursa hii kuwatanabahisha waislam wote waliomo jamii forum, ya kuwa tumefikiwa na mwezi mtukufu wa Ramadhani. Mwezi huu ni kwa ajili ya kufunga na kuzidi kujikurubisha kwa ALLAAH, kwa kuswali, kusoma Quran kwa wingi, kutoa swadaqa, zakkah, kuzidisha kila aina ya jambo jema ulioamrishwa na Mola wako.

Pia vilevile kuacha Yale yote ALLAAH aliyotukataza, kusema uongo, kusenganya, kuiba, kulumbana (kugombana) n.k

Na vilevile kuacha kupoteza muda kwa mambo ya upuuzi:- karata, misalsala, kulala sana, bao, muda mwingi kukaa kwenye t.v na computer, kuchezea simu n.k.

Hii fursa tulioipata ni adhiym kwa kila muislam iliyomfikia, kwa ajili ya kuomba msamaha kwa ALLAAH, na kukubaliwa toba zetu.

Kwani ALLAAH ametuahidi yoyote atakaefunga kwa imaanan na Ucha Mungu basi ALLAAH atamsamehe madhambi yake, kwa hivyo tufanyeni jitihada sana kwa kutaraji kusamehewa dhambi ZETUna muumba.

KILICHONISUKUMA KUANDIKA UZI HUU, NIMEONA KUWA KUSHAANZA KUTOKEA NA BAADHI YA THREAD AMBAZO ZIMEANZA KULETA UPOTOSHAJI JUU YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN, (mfano kumekucha Zanzibar ) NA WATU KUANZA KULUMBANA. SISI WAISLAM TUSIJIINGIZE KABISA KATIKA MALUMBANO HAYO NA WALA TUSIZISOME KABISA THREAD HIZO KWA MAANA ZINAWEZA KUPELEKEA KUHARIBU SWAUMU ZETU NA LENGO LA KUFUNGA TUKALIKOSA.

HATUWEZI KUJUA WENYE KUFANYA HIVYO WAMETUMWA AU NI AKILI ZAO WENYEWE TUU.
TUNAMUUOMBA ALLAAH ATUJAALIE TUFUNGE SALAMA NA SWAUMU ZETU ZIWE ZENYE KULUBALIWA.
AMIYN

Hii thread si ya majibizano ni TANBIHI kwa waislam
 
Mashaallah, leo katika msikiti wangu wakitaa ulijaa hadi safu zamwisho, wakati tulikuwa tunaswali swafu mbili hadi tatu. Nawaombea kwa Allah awajalie waendelee na ibada hawa ndugu zetu hata baada ya ramadhani.


Ramadhani Mubarak.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…