[emoji120] [emoji120] [emoji120]Sawa umeeleweka
Umesomeka jamaamkuu acha uchochezi kufunga imeamriwa na Allah
Quran 2:183 Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga saumu kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu.
japo Aya hapo juu inatuambia kuwa, kumbe kufunga kwa ndugu zetu hawa ni kwa kulazimishwa na sio hiyari yao sasa:
1. Wapi tunasoma katika Taurat kuwa Adam alifunga Saumu/Ramadhani?
2. Wapi tunasoma katika Taurat kuwa Musa alifunga Saumu/Ramadani?
3. Wapi tunasoma katika Taurat kuwa Ibrahim alifunga Saumu/Ramadhani?
MAONI YANGU MSIJIFANYE WACHAMUNGU KIPINDI CHA KUFUNGA TU ILA MUENDELEE SIKU ZOTE KUEPUKA MATENDO MAOVU
Mkuu sala haiondoi fungaCha kuwakumbusha ndugu zanguni, mfungo wa ramadhani sio adhabu ila ni nafasi mola wetu mlezi anatupa ili tujikurubishe kwake na kumuomba msamaha na kuomba rehma na kuwekwa mbali na moto wa jehanamu,
Funga inaendana na SALA, kama Husali ndugu zangu basi hakika wewe unashinda na njaa wala hupati thawabu zozote zaidi ya kujiongezea mzigo wa dhambi, nasisitiza tena FUNGA inaenda sambamba na SALA 5.
Sala ndio sehemu pekee ya mja kuongea na Mola wake, tuache uvivu kipindi hiki, tuamkeni usiku na kujipendekeza kwa mola wetu, mwezi ni mmoja tu, hivyo tuutumieni ipasavyo, omba chochote kwa Mola wako, mwambie chochote anakusikia.
Tukatazane mabaya na tuamrishane yaliyo mema.
Mkuu sala haiondoi funga
Hizo ni ibada mbili tofauti
Ila inashauriwa ukifunga uswali maana utapata thawabu nyingi sana
Ila ukifunga na usiswali funga yako inakubalika kama kawaida cha muhimu uwe umetia nia na umejizuia na yale yote yanayotengua funga.
Mzee wa vitasa nawatakia mfungo mwema wa ramadhan....Mungu atuongoze inshaalah .
Mkuu hili suala limekuwa likileta mkanganyiko mkubwa sana baina ya wanazuoniSWALI:
Ipi hukumu ya mwenye kufunga Ramadhwaan bila ya Swalaah au akaswali katika Ramadhwaan na haswali (miezi) mingine?
JIBU:
Ama Swawm yake, Zakaah yake, Hajj yake au yasiyokuwa hayo katika ´amali zake bila ya Swalaah hazitomfaa. Kwa kuwa la sahihi ni kuwa mwenye kuacha Swalaah ni kafiri, kutokana na dalili maalumu, miongoni mwazo ni Hadiyth: "Ahadi iliyoko baina yetu na wao (makafiri) ni Swalaah, mwenye kuiacha amekufuru."
Na Hadiyth: "Baina ya mtu na kafiri na shirki ni kuacha Swalaah."
Hadiyth hizi mbili ni sahihi na dalili zake ziko wazi.
Hadithi ndio hizo nimekupa, kazi kwako sasa kuzipitia kwa utulivu, "Tofauti yenu na wao ni SALAH"Mkuu hili suala limekuwa likileta mkanganyiko mkubwa sana baina ya wanazuoni
Wapo wanaodai ukifunga na usiposwali ,funga yako itakuwa ni batili na wana hoja zao kuhusu hilo
Pia wapo wanaodai ukifunga na usiposwali funga yako inakubalika kama kawaida na hawa pia wana hoja zao mf wa moja za hoja zao.
Hawa wanadai funga na swala ni nguzo mbili tofauti katika zile nguzo tano za uislamu
1)Kutoa shahada
2) kuswali
3)kutoa zakka
4)kufunga mwezi mtukufu wa ramadan na
5)kuhijji makka kwa wenye uwezo