Ramadhan Special Thread

Asalam àleykum..

Mimi ni kijana wa kiislam Je kutumia maneno kama baby , honey, my love na mengine yenye lengo la kumaanisha ni wapenzi hali ya kuwa sijamtolea barua ikiwa nimefunga funga yangu itaswii?..

Je ikiwa nimeshamtolea barua na nimejibiwa kuwa nimekubaliwa kumuoa kutumia maneno kama hayo funga yangu itaswii?
 
Swali jaman nilikuwa na mpenzi muislamu nikiwa period haniruhusu kushika kanzu zake hii maana yake Nini?
Kwanza kuwa na mpenzi asiekuwa mume wako hairuhusiwi kisheria na imani ya kiislam.
Sasa hapo nashindwa kumuelewa ana imani gani?
Dini ina misingi yake na taratibu zake na kuwa na mpenzi bila ndoa ni haram period
 
Swali jaman nilikuwa na mpenzi muislamu nikiwa period haniruhusu kushika kanzu zake hii maana yake Nini?

Huyo mpenzi wako,inaonekana haujui uislamu vizuri.

Almuhimu alikuwa anafanya kosa kuishi na mwanamke pasi na ndoa

Swali lako linajibiwa kwa mizani ya ndoani,kwani tukiliacha nje ya ndoa ni makosa juu ya makosa. Kwa ufupi hakuna mahusiano kati ya kushika kanzu na damu ya hedhi,nje ya hapo ni imani za kishirikina na ujinga.
 
Kuhusu funga kama funga ni sahihi inasihi na wala haibatiliki

Lakini kwa hayo maneno ya kuchombeza haifai kumtamkia kwa sababu bado hajawa mkeo na hakawa halali yako kwa maana haujapita ihalalisho wa kisheria atabaki kuwa mchumba na mchumba wako ni kama wanawake wengine ambao sio wachumba zako kwa maana hufai kufanya nae muamala wowote wa kimapenzi na yeye.

Hilo la kumuita hayo majina linaweza kupelekea fitna na kuanza mazungumzo yasiyo na staha na mtu ambaye bado hajawa mkeo.

Saumu ni sahihi lakini kitendo cha kuitana majibu matamu matamu kabla ya ndoa ni makosa ambayo hayabatilishi saumu.
 
Naam, hapa iko faida, kwa maana kuna kukumbushana na pia kuna kuamrishana mema na kukatazana mabaya.
 
Mkuu mimi ni muislamu sema kuna rafikiyangu alinionjesha kitimoto yani natamani kuachakula lakini siwezi kabisa huyu mdudu nimtam sana aise
Mkuu, uislam ni kufuata maamrisho na kuacha makatazo ya Allah, na si kufuata matamanio ya nafsi yako.
Kwa hiyo acha kitimoto kwa ajili ya Allah naye atakupa jambo zuri mno kuliko hicho kitimoto.
 
Kuna katazo gani la kutumia emoji ya mikono ?

Kuaema halina asili peke yake haitoshi kuonesha haifai.

Kuna katazo gani kutumia emoji za mikono mkuu?
 
Basi wewe endelea kula mkuu wala usijipe shida.
Tena kama "utafunga" basi muda wa futari au daku unapata na kitimoto chako saaafii.
Kama nilivyoandika awali...'mwisho wa yote wewe ndio utawajibika kwa matendo yako'.
Tuamrishane mema na kukatazana mabaya, mpe nasaha badala ya kuzidi kumsukumiza kwenye uasi, kwani yeye kuacha uovu kwa ushawishi wako ni jambo bora sana kwako pia.
 
Swali jaman nilikuwa na mpenzi muislamu nikiwa period haniruhusu kushika kanzu zake hii maana yake Nini?
Demiss huyo alikuwa hajitambui, kwa maana kaona wewe kushika kanzu yake ni tatizo lakini mahusiano yenu yaliyo nje ya sheria kaona ni poa tu!, huyu hajitambui na pia haujui uislam wake pia.
 
Tuamrishane mema na kukatazana mabaya, mpe nasaha badala ya kuzidi kumsukumiza kwenye uasi, kwani yeye kuacha uovu kwa ushawishi wako ni jambo bora sana kwako pia.
Huyo jamaa hayupo hapa kwa ajili ya kujifunza mkuu bali kufanya mzaha na kuharibu maudhui ya mjadala.
Huu ni uzi maalum kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani lakini yeye analeta habari za kitimoto tena akijinisabu kwamba yeye ni Muislam na bado anajiuliza ima afunge au la maana atamisi hicho kitimoto chake!!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…